Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkutugenzi wa
Ufundi, Bw. McJohn Mbiri (kulia Kwake) kuhusu mitambo ya kuzaisha
gesi ya hewa ya ukaa wakati alipotembelea kiwanda cha TOL Limited
kilichopo katika kijiji cha Ikama wilayani Rungwe Julai 30, 2017. Kushoto
kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla.
NA OWM,RNGWE
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewasihi Watanzania wanaofanya kazi
katika viwanda mbalimbali nchini kufanya kazi kwa bidii na kuwa waaminifu.
Amesema Tanzania imedhamiria kukuza uchumi wake kupitia sekta ya
viwanda hivyo ni vema watakaopata fursa ya ajira katika viwanda hivyo kuwa
waadilifu.
Ameyasema hayo leo (Jumapili, Julai 30, 2017) wakati akizungumza
na wafanyakazi wa kiwanda cha gesi cha Ikama kilichoko wilayani Rungwe.
Waziri Mkuu amesema wakati Serikali ikiendelea kuwakaribisha
wawekezaji nchini, wananchi walioajiriwa kwenye maeneo hayo wawe waaminifu.
“Mnatakiwa muwe waaminifu, msibebe kitu chochote ndani ya
kiwanda bila ya ridhaa ya wamiliki kwa kuwa mtaonyesha taswira mbaya kwa
wawekezaji.”
Amesema uaminifu wao ndio utawezesha Watanzania wengi kupata
ajira kwenye viwanda hivyo ambavyo vimejengwa katika maeneo yao.
Awali, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa kiwanda hicho kinachomilikiwa
na kampuni ya TOL Gases, Mhandisi Harold Temu alisema kiwanda kinauwezo
wa kuzalisha tani 46 kwa siku.
Alisema gesi inayozalishwa kiwandani hapo ni ya Carbon Dioxide
ambayo inauzwa nchini na nchi jirani za Zambia, Malawi, Zimbabwe na Congo.
Mhandisi Temu alisema wateja wakubwa wa gesi hiyo ni viwanda vya
kutengenezea soda, bia na pia hutumika katika kuhifadhia chakula na kwenye
vifaa vya kuzimia moto.
Mapema Waziri Mkuu alitembelea kiwanda cha kuchakata majani ya
chai cha Katumba, ambapo alisema Serikali inaimarisha Ushirika wa zao hili ili
wakulima waweze kupata tija.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea kiwanda cha chai cha Katumba wilayani
Rungwe Julai 30, 2017. Kulia ni Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla na
kushoto ni Meneja Uzalishaji wa kiwanda hicho, Ramadhani Kampasili.
Waziri
Mkuu,Kassim Majaliwa akitazama chai iliyosindikwa na kufungashwa tayari
kwa kuuzwa wakati alipotembelea kwianda cha chai cha Katumba wilayani Rungwe
Julai 30, 2017.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa umma wa wilaya ya Rungwe
Julai 30, 2017. Kulia ni Naibu Spika, Dkt. Tulia Ackson na kushoto ni Mkuu wa
mkoa wa Mbeya Amos Makalla.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi wa kiwanda cha gesi cha TOL
Gasese Limited kilichopo katika kijiji cha Ikama wilayani Rungwe Baada ya
kuwasili kiwandani hapo Julai 30, 2017 Kushoto ni Naiobu Spika wa Bunge, Dkt.
Tulia Ackson.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana viongozi wa kiwanda cha chai cha Katumba
wilayani Rung wakati alipowasili kiwandani hapo kukagua shuguli za kiwanda
hicho Julai 30, 2017.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa Rungwe baada ya kutembelea
kiwanda cha Chai cha Katumba Julai 30, 2017.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia ngoma ya asili baada ya kuwasili kwenye uwanja
wa michezo wa Kandete katika jimbo la Busokelo mkoani Mbeya
kuhutubia mkutano wa hadhara Julai 30, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wazee wa Busokelo baada ya kuwasili kwenye uwanja wa michezo wa Kandete katika jimbo la Busokelo kuhutubia mkutano w








No comments :
Post a Comment