KUMEKUWEPO na upotoshaji wa mafunzo ya utarajali (Internship programme)
bila malipo yaani fedha za kujikimu wakati wa mafunzo hayo kwa baadhi ya
wanaotarajia kuanza mafunzo kwa vitendo mapema mwaka huu.
Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto inapenda
kuwajulisha kwamba kwa sasa hakuna ‘intern’ aliyepangiwa kuanza mafunzo hayo
kwani tunasubiri watoke waliopo kwenye mafunzo.
Barua iliyodukuliwa na kusambaa kwa lengo la kupotosha wataraji hao
ilikuwa ni kwa ajili ya wataraji (intern) kutoka nje ya nchi ambao kwa sheria
hawalipiwi na Serikali ya Tanzania.
Aidha wapo ‘intern’ wawili ambao wanasoma nchini China na mwingine
Algeria masomo yao yalihitaji mafunzo kwa vitendo kabla ya kumaliza na kwa kuwa
ilikua lazima warudi vyuoni mwezi Oktoba waliomba kufanya mafunzo hayo kwa kujigharimia pamoja na kuwa ni watanzania na wazazi wao
walikuwa wameridhia hilo kwa maandishi ili warudi mapema kumalizia program yao ya udaktari.
Hivyo ni watanzania wawili tu wameshapata barua yenye kuwataka kujilipia kwa mazingira hayo hakuna wengine
waliyepewa barua ya kuruhusiwa kwenda mafunzo ya utarajali (internship) bila
malipo.
Imetolewa na;
Nsachris Mwamwaja
Mkuu Kitengo cha
Mawasiliano Serikali-Afya
30/7/2017

No comments :
Post a Comment