Maafisa wa Mfuko wa PSPF kulia Faidha
Khatau na Hazina Konde wakimkabidhi mashukaka Mkurugenzi Mtendaji wa
Hospitali ya Mnazi Mmoja Dr Ali Salum Ali anayefutia ni Mkurugenzi
Utawala na Uendeshaji Dr. Abubakar Khamis Hamadi, hafla hiyo imefanyika
katika ukumbi wa jengo jipya wa Hospitali ya Watoto Mnazi mmoja PSPF
imekabidhi mashuka 75 kwa ajili ya wodi za watoto katika hospitali hiyo
Kuu Zanzibar ikiwa ni moja ya kusaidia Jamii.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya
Mnazi Mmoja Zanzibar Dr. Ali Salum Ali akipokea mashuka kutoka kwa
Maafisa wa Mfuko wa PSPF Tawi la Zanzibar Bi Hazina Konde (katikati) na
Afisa Mkuu wa Tawi la Zanzibar PSPF Bi. Faidha Thatau wakikabidhi
mashuka hayo kwa ajili ya matumizi ya Wodi ya Watoto katika hospitali ya
Taifa ya Mnazi Mmoja Zanzibar hafla hiyo imefanyika katika majengo
mapya wa hospitali hiyo Zanzibar.
Afisa Mfawidhi wa Mfuko wa PSPF Tawi la
Zanzibar Bi Faidha Thatau akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi
mashuka kwa Uongozi wa Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Zanzibar. Mfuko wa
PSPF hutowa huduma za mafao mbalimbali kwa Wanachama wake Bima ya Afya
kwa wateja wao.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali Kuu ya
Mnazi Mmoja Zanzibar Dr. Ali Salum Ali akitowa shukrani kwa Uongozi wa
Mfuko wa PSPF kwa msaada wao huo na kuwataka isiwe mwisho iwe ni
endelevu kwa kutoa misaada mbalimbali kwa hospitali hiyo uwezo
ukiruhusu.
Afisa Mfawidhi wa Mfuko wa PSPF Bi.
Faidha Khatau akigawa vipeperushi vya maelezo ya PSPF kwa viongozi wa
Hospitali ya Mnazi Mmoja kujuwa huduma zinazotolewa na Mfuko huo.
Viongozi wa Hospitali ya Mnazi Mmoja
wakifuatilia vipeperushi vya Mfuko wa PSPF baada ya kukabidhiwa kupata
maelezo ya PSPF, wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa mashuka kwa
ajili ya Wodi ya Watoto Zanzibar.
Afisa Mfawidhi Mfuko wa PSPF Tawi la
Zanzibar kulia Bi Faidha Khatau akimkabidhi mashuka Afisa Muunguzi
katika Wodi ya Watoto Hospitali ya Mnazi Mmoja Bi. Fatma Ali Mzee na
kushoto Afisa Mfawidhi Msaidizi Bi Hazina Konde, wakiwa katika moja ya
Wodi ya Watoto katika hospitali mpya ya Watoto Mnazi Mmoja.
Maafisa Wafawidhi wa PSPF Tawi la
Zanzibar wakitandika kitanda katika moja ya vitanda katika Wodi ya
Watoto Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar baada ya kukabidhi mashuka hayo
75 kwa ajili ya hospitali hiyo ya Watoto Zanzibar.
Maafisa Wafawidhi wa PSPF Tawi la
Zanzibar wakitandika kitanda katika moja ya vitanda katika Wodi ya
Watoto Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar baada ya kukabidhi mashuka hayo
75 kwa ajili ya hospitali hiyo ya Watoto Zanzibar.
Maafisa wa Mfuko wa PSPF Tawi la
Zanzibar wakitoka katika jengo ya hospitali ya Watoto Mnazi Mmoja baada
ya kumalizika kwa hafla ya kukabidhi msaada wa mashuka kwa ajili ya
matumizi ya Wodi ya Watoto Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Zanzibar.
Imetayarishwa na OthmanMapara.Blogspot.com.
Email othmanmaulid@gmail.com
Mobile.0777424152.
No comments :
Post a Comment