Saturday, July 1, 2017

BENKI YA DUNIA YAIPATIA TANZANIA MKOPO WA DOLA MILIONI 180 KUBORESHA ELIMU BILA MALIPO

unnamed
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James (Kushoto) na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia anayehudumia nchi za Tanzania, Somalia, Malawi na Burundi, Bella Bird, wakitia saini makubaliano ya Benki ya Dunia kuipatia Tanzania mkopo wenye riba nafuu wa Dola za Marekani milioni 80 kwa ajili ya kutekeleza maboresho ya elimu ya msingi na sekondari kupitia mpango wa  lipa kwa matokeo (elimu bila malipo), Jijini Dar es Salaam
1
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James (Kushoto) na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia anayehudumia nchi za Tanzania, Somalia, Malawi na Burundi, Bella Bird, wakitia saini makubaliano ya Benki ya Dunia kuipatia Tanzania mkopo wenye riba nafuu wa Dola za Marekani milioni 80 kwa ajili ya kutekeleza maboresho ya elimu ya msingi na sekondari kupitia mpango wa  lipa kwa matokeo (elimu bila malipo), Jijini Dar es Salaam.
2
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James (Kushoto) na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia anayehudumia nchi za Tanzania, Somalia, Malawi na Burundi, Bella Bird, wakibadilishana hati (mkataba) ya mkopo wenye riba nafuu wa Dola za Marekani milioni 80 kwa ajili ya kutekeleza maboresho ya elimu ya msingi na sekondari kupitia mpango wa  lipa kwa matokeo (elimu bila malipo), jijini Dar es Salaam.
3
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw, Doto James akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) baada ya kutia saini makubaliano na Benki ya Dunia ya kuipatia Tanzania mkopo wenye riba nafuu wa Dola za Marekani milioni 80 kwa ajili ya kutekeleza maboresho ya elimu ya msingi na sekondari kupitia mpango wa  lipa kwa matokeo (elimu bila malipo), Jijini Dar es Salaam.
4
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Simon Msanjila (kulia) pamoja na baadhi ya maafisa waandamizi wa Serikali wakishuhudia tukio la kutiwa saini kwa mkataba wa mkopo wa riba nafuu wa Dola za Marekani milioni 80 (shilingi bilioni 180) uliotolewa na Benki ya Dunia kwa ajili ya kugharamia mpango wa kuboresha elimu kupitia program ya lipa kwa matokeo (elimu bila malipo), Jijini Dar es Salaam.
5
Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia anayehudumia nchi za Tanzania, Somalia, Malawi na Burundi, Bi. Bella Bird, akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) baada ya kusaini makubaliano ya Benki yake ya kuipatia Tanzania mkopo wenye riba nafuu wa Dola za Marekani milioni 80 kwa ajili ya kutekeleza maboresho ya elimu ya msingi na sekondari kupitia mpango wa  lipa kwa matokeo (elimu bila malipo), Jijini Dar es Salaam.
6
Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia anayehudumia nchi za Tanzania, Somalia, Malawi na Burundi, Bi. Bella Bird, akisisitiza jambo mbele ya  waandishi wa habari (hawapo pichani) baada ya kusaini makubaliano ya Benki yake ya kuipatia Tanzania mkopo wenye riba nafuu wa Dola za Marekani milioni 80 kwa ajili ya kutekeleza maboresho ya elimu ya msingi na
sekondari kupitia mpango wa  lipa kwa matokeo (elimu bila malipo), Jijini Dar es Salaam.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)
……………………
Benny Mwaipaja, WFM-Dar es Salaam
BENKI ya Dunia imeipatia Tanzania mkopo wenye masharti nafuu wa Dola za Marekani milioni 80 kwa ajili ya kusaidia mpango wa Serikali wa miaka 11 wa Elimu bila malipo kuanzia elimu ya msingi hadi sekondari nchini.
Kiasi hicho cha fedha ni nyongeza ya Dola milioni 122 zilizotolewa na Benki hiyo katika awamu ya kwanza ya utekelezaji wa maboresho ya elimu kupitia Mpango wa Tekeleza kwa Matokeo Makubwa sasa-BRN, uliolenga kuondoa changamoto za elimu nchini.
Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia anayehudumia nchi za Tanzania, Somalia, Malawi na Burundi, Bella Bird amesema wakati wa utiaji saini mkataba wa nyongeza ya fedha hizo kati yake na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James, kuwa nyongeza ya Dola milioni 80 imetokana na Benki hiyo kuridhishwa na namna Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Dokt. John Pombe Magufuli, ilivyosimamia kikamilifu mpango huo wa utoaji elimu bure na kuwanufaisha wanafunzi wengi wakiwemo wanaotoka katika familia masikini.
Amesema kuwa uamuzi huo umesababisha ongezeko kubwa la wanafunzi wanaojiunga na elimu ya msingi, kuongezeka kwa ufaulu, wanafunzi kujua maarifa ya hesabu, kusoma na kuandika, utoaji wa ruzuku  ya elimu kwa wakati, hatua ambayo pia imesababisha kuwepo kwa changamoto za ukosefu wa miundombinu ya shule, changamoto ambazo anaamini zinapungua kupitia mkopo huo wenye masharti nafuu.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James ameishukuru Benki ya Dunia kwa kutoa fedha hizo ambazo amesema zitasaidia kwa kiasi kikubwa mipango ya Serikali ya kuboresha elimu nchini na kuondoa changamoto zinazoukabili mpango huo likiwemo ongezeko hilo kubwa la wanafunzi.
Bw. James ameeleza kuwa fedha hizo zitasaidia ujenzi wa miundombinu ya madarasa, ubora wa eimu, ukaguzi wa shule, upelekaji wa walimu, na kuwasaidia wanafunzi wenye mahitaji maalumu ili waweze kupata haki hiyo ya msingi ya elimu.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Simon Msanjila, amesema kuwa katika awamu ya kwanza ya utekelezaji wa mradi wa elimu wa lipa kulingana na matokeo upitia mkopo wenye masharti nafuu wa Dola za Marekani milioni 122 zimetumika kujenga madarasa 1,400, matundu 3,390 ya vyoo, mabweni 261, majengo ya utawala 9, mabwalo ya chakula 9 nyumba za walimu 11, uchimaji wa visima vya maji katika shule nne na kukarabati vyuo vya ualimu.
Amesema kuwa  mkopo mpya wa dola za Marekani milioni 80 uliotolewa na Benki ya Dunia hata kabla ya awamu ya kwanza ya mradi huo kumalizika hapo mwakani, umeonesha nia ya dhati ya Benki ya Dunia kusaidia maendeleo ya elimu nchini.

No comments :

Post a Comment