Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina amewataka viongozi
wilaya ya Ilala kuwachukulia hatua kali watu wanaokaidi kutunza
mazingira yanayowazunguka.
Ameyasema hayo mapema hii leo jijini Dar es salaam alipokuwa akishiriki katika zoezi la usafi wa kila mwisho wa mwezi.
Amesema kuwa ili kuweza
kuhakikisha zoezi hilo linatimia na kuwashirikisha wananchi wote,
ni
lazima viongozi wawachukulie hatua kali wananchi ambao wanakaidi
kushiriki katika zoezi hilo kwa lipo kwaajili ya kuiokoa jamii na
magonjwa mbalimbali ya mlipuko.
“Ninyi viongozi mnatakiwa
kuwachukulia hatua kali wale wananchi wachache wanaokaidi kushiriki
katika usafi, kwani haiwezekani watu wailaumu Serikali kwa kila kitu,
sisi viongozi wa juu tuleteeni wale walioshindikana ili tuweze
kuwashughulikia,”amesema Luhaga.
Aidha, katika hatua nyingine,
Luhaga amewataka wananchi kuunga mkono hatua za zinazochuliwa na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli kwani anania ya
dhati kuleta maendeleo ya nchi.
Hata hivyo, pamoja na hayo, Mpina
ameongeza kuwa katika awamu hii ya TanoTanzania imepata Rais wa kipekee
ambaye amekuwa mfano wa kuigwa barani Afrika na duniani kote
No comments :
Post a Comment