Ikiwa
ni katika kuboresha mazingira na kuepukana kutaka miti zipo njia nyingi
sana za kuhakikisha mazingira yanaendelea kutunzwa na kuboreshwa,
Kampuni ya Afri Tea and Coffee Blenders imekuja na suluhisho la kuachana
na masuala ya ukataji miti ovyo.
Watanzania
wametakiwa kubadilika kwa kuacha kukata miti ovyo kwa ajili ya mkaa
bali watumie nishati mbadala ambayo itasaidia katika kutunza mazingira.
Hayo yamesemwa wakati akizungumza na Globu ya Jamii, Mkuu wa Masoko na Biashara wa Afri Tea and Coffee Blenders (ATCB)Zachy
Mbenna amesema wamekuja na njia mbadala ya kuepukana na matumizi ya
mkaa kwa kutengeneza nishati mbadala inayotengenezwa kwa mabaki ya miti
(magome) aina ya miwati.
Mbenna
amesema, utumiaji wa magome hayo katika utengenezaji wa nishati mbadala
umechukua nafasi ya ukataji miti hai ambapo watu wanatumia kutengeneza
mkaa na kupelekea kuharibu mazingira.
"Nishati
hiyo mbadala ambayo inajulikana kama Briquets inatengenezwa kwa magome
ya mabaki ya miti ya miwati ambayo inatumika kwa ajili ya kutengenezea
ngozi, tulifikia hatua hii ya kutengeneza hizi baada ya kuona tunatumia
zaidi ya tani nyingi zaidi za kuni ndani ya mwezi mmoja kitu ambacho
kilikuwa kinatugharimu sana,"amesema Mbenna.
"Baada
ya kuona tumefanikiwa katika kupunguza gharama pamoja na ukataji wa
miti kwa ajili ya kuni, baadhi ya viwanda navyo kutumia bidhaa hizi
tukaamua kupeleka kwa wananchi kwa matumizi ya nyumbani ikiwemo pamoja
na kuja na majiko yao maalumu kwani Briquets zinahitaji hewa ili kuweza
kufanya kazi kwa uharaka zaidi, "amesema Mbenna.
Ametoa
wito kwa makampuni, taasisi na watu wengine watambue wao ndiyo watu wa
kwanza wa kulinda mazingira na njia nzuri ni kutumia nishati mbadala
ambayo ni njia bora ya kuhifadhi mazingira.
Mkuu
wa Masoko na Biashara wa kampuni ya Afri Tea and Coffee Blenders (ATCB)
akielezea mkaa na aina ya majiko yanayotumika kwa nishati mbadala
(Briquets) zinazotengenezwa kampuni ambapo yanapatikana kwenye maonesho
ya 41 ya kimataifa ya biashara ya sabasaba yanayoendela Jijini Dar es
salaam.
Mkuu
wa Masoko na Biashara wa kampuni ya Afri Tea and Coffee Blenders (ATCB)
akionyesha mkaa na aina ya majiko yanayotumika kwa nishati mbadala
(Briquets) zinazotengenezwa kampuni ambapo yanapatikana kwenye maonesho
ya 41 ya kimataifa ya biashara ya sabasaba yanayoendela Jijini Dar es
salaam.
Fundi
wa majiko yanayojulikana kama Simba Stones akielezea namna nishati
mbadala ya mkaa wa magome ya miti (Briquets) inavyofanya kazi kwnye
majiko hayo yanayopatikana kwenye maonesho ya 41 ya kimataifa ya
biashara ya sabasaba yanayoendela Jijini Dar es salaam.
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Mtaalamu
na mshauri wa masuala ya urembo na Ngozi Irene Moshi ametoa ushauri kwa
kina mama hususani wasichana kutumia vipodozi vyenye vimea asilia ili
kuepukana na kuharibu ngozi zao.
Amesema hayo
wakati akiongea na globu ya Jamii, Irene amesema kupitia saluni ya
Timeless wameweza kuwasaidia watu wengi na kuwapatia tiba kuhusiana na
masuala ya ngozi na hasa katika usahihi wa kutumia vipodozi
vinavyoendana na ngozi ya muhusika.
"Tunatoa
ushauri wa kitaalamu kuhusiana na matumizi sahihi ya vipodozi kulingana
na aina ya ngozi ya muhusika pia kutoa malekezo ya kutumia vitu sahihi
kwa wakati sahihi kama vile kulingana na hali ya hewa kipindi cha joto
na baridi,"amesema Irene.
Amesema
kuwa, anatoa ushauri kwa vijana hususani wa kike kujifunza zaidi
masuala ya urembo kwani inaweza kusaidia katika kuboresha ngozi zao na
wanaweza kutumia vipodozi sahihi na kutokuharibu ngozi zao.
Mbali
na kutoa tiba, Timeless walianza kutoa mafunzo rasmi mwaka 2016 Irene
amesema kuwa wanatoa mafunzo kwa vijana wanaopendelea kufahamu shughuli
mbalimbali za urembo ikiwemo tiba ya ngozi, upambaji ambapo wameweza
kutoa vijana wengi kwa kipindi cha mwaka mmoja na tayari wengine
wameshajiajiri katika sehemu zao na pia Timeless wanajishughulisha na
masuala ya kupamba maharusi, nywele na kucha na mapambo ya maharusi
ikwemo kadi.
Mtaalamu
na mshauri wa masuala ya urembo na Ngozi Irene Moshi akimuhudumia mteja
aliyetembelea katika banda lao la Timeless Hair and Beauty Saloon
kwenye maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa katika viwanja vya
Sabasaba Jijini Dar es salaam.
Mtaalamu
na mshauri wa masuala ya urembo na Ngozi Irene Moshi akizungumza na
Globu ya Jamii kuhusiana na masuala ya urembo wa ngozi na kuonyesha
baadhi ya mapambo ya maharusi yanayopatikana kwenye saluni yao ya
Timeless.
Wateja wakiwa wanapata maelezo kutoka kwa mfanyakazi wa Timeless Hair and Beauty Saloon katika banda laokwenye maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa katika viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es salaam.
(Picha na Emanuel Massaka).
No comments :
Post a Comment