Na Ripota wa Mafoto Blog, Kibaha
MBUNGE wa Kibaha mjini, Silyvestry Koka (kulia) na Diwani wa Kata ya Sofu, Yusuf Mbonde, wakishirikiana na wananchi wa kata hiyo Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani, kusafisha eneo lililo na majani kwa ajili ya maandalizi ya ujenzi wa Zahanati. Mhe. Mbunge leo asubuhi alifanya ziara ya kushitukiza katika eneo hilo baada ya kupata tetesi kuwa eneo hilo limeuzwa.
Aidha imeelezwa kuwa tetesi za kuuzwa kwa eneo hilo zilimfikia Diwani wa Kata hiyo, Bw.Mbonde, aliyeamua kumfuata Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji Kibaha, Jenifer Ommolo, ambaye 'eti' alikiri kuwa jambo hilo nalitambua na kumwahidi kuwa wangepewa eneo mbadala wa hilo, jambo ambalo Diwani hakukubariana nalo na kuamua kulifikisha kwa Mhe.Mbunge wake.
Mbunge huyo, alifika eneo hilo na kukutana na wapiga kura wake na kuamua kushiriki nao zoezi la kusafisha baada ya baadhi ya wananchi kukumbwa na hofu wakidai kuwa eneo hilo lilibadilishwa lengo la matumizi kwa kumgawia mtu aliyejulikana kwa jina la Mchome, ili kuliendeleza, ambaye pia hadi Mbunge anafika leo alikuwa bado hajaanza ujenzi wa aina yeyote.

Imeelezwa
kuwa eneo hilo baada ya kutolewa kwa ajili ya kujengwa Zahanati ambayo
kwa kiasi kikubwa ilitakiwa kujengwa kwa ushirikiano mkubwa na wananchi
ambao wengi wao walipigwa na butwaa na kurudi nyuma baada ya kusikia
eneo hilo amegaiwa Mchome, aliyetakiwa kuliendeleza.
Baada
ya Mbunge Koka kuwasili eneo hilo hii leo asubuhi, wananchi wajitokeza
na kuonyesha ushirikiano huo kwa kushirikiana na viongozi wao, na
baadaye kubaki na matumaini ya kuona kinajengwa kile walichokikusudia
baada ya Mbunge kutoa tamko kwa kusema eneo hilo linatakiwa kujengwa
Zahanati ya wananchi na si kitu kingine.
Mbunge
wa Kibaha mjini, Silyvestry Koka, akizungumza na wananchi wa Kata ya
Sofu Wilayani Kibaha, wakati wa zoezi la kufyeka na kusafisha eneo la
kujenga Zahanati,ambapo alilaani kitendo hicho cha uuzwaji wa eneo la
wananchi alichokiita cha kitapeli.
Wananchi wakimsikiliza kwa makini mbunge wao, baada ya zoezi hilo.

No comments :
Post a Comment