Waziri
wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango. (kushoto), akikaribishwa na
Afisa Udahili wa Chuo Cha Uhasibu Arusha, (IAA), Bw. Gerald Malisa,
alipofika kutembeela banda la chuo hicho lililoko jengo la Wizara ya
Fedha na Mipango, kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere, maarufu Sabasaba,barabara
ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa
ya Dar es Salaam yanaendelea kwenye viwanja hivyo na yatafikia kilele
Julai 13, baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John
Pombe Magufuli, kuomba Tan Trade waongeze siku tano zaidi ili kutoa
fursa pana kwa wanachi kutembelea maonesho hayo na kupata faida
mbalimbali.
Mkuu
wa Mawasiliano ya Serikali Wizara ya Fedha na Mipango, Bw.Ben Mwaipaja,
(kushoto), na mama huyu wakitembelea banda la Chuo hicho Julai 9, 2017.
Mkuu
wa Mawasiliano ya Serikali Wizara ya Fedha na
Mipango, Bw.Ben Mwaipaja, (wapili kulia), na maafisa wa chuo cha IAA,
Bi.Sekunda Titus, (kushoto) na Bw. Gerald Malisa, (wapili kushoto),
wakimsikiliza Afisa Uhusiano na Masoko wa
chuo hicho, Bi.Sarah Goroi, (kushoto)9, 2017.
Afisa Uhusiano na Masoko wa
chuo Uhasibu Arusha, (IAA), Bi.Sarah Goroi(wapili kushoto), akiwa na Afisa
Utawala wa chuo Bi. Sekunda Titus,(kushoto), wakimpatia maelezo ya
programu mbalimbali zitolewazo na chuo hicho, muhitimu wa shahada ya
kwanza ya Sayansi ya Kompyuta,(bachelor degree in computer science),
Bw.Jacob Stephene Siray, alipotembeela banda la chuo hicho Julai 9,
2017. Bw. Siray ni muhitimu katika chuo hicho mwaka 2016.
Afisa
Uhusiano na Masoko wa
chuo hicho, Bi.Sarah Goroi, (kushoto), akiendelea kutoa ufafanuzi wa
huduma za elimu ya juu inayotolewa kwenye chuo hicho kwa vijana hawa
waliotembeela banda la PSPF Julai 9, 2017.
Afisa Uhusiano na Masoko wa
chuo hicho, Bi.Sarah Goroi(kushoto), akimsikiliza kijana huyu aliyefika kwenye banda la chuo hicho Julai 9, 2017.
Mkurugenzi
wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA, anayeshughulikia masuala ya
habari na utangazaji, Bw. Freddy Ntobi, (kulia), akitembelea banda la
chuo hicho Julai 9, 2017.
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango ametembeela
banda la Chuo Cha Uhasibu Arusha, (IAA), lililoko kwenye jengo la Wizara ya Fedha na
Mipango kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam kunakofanyika
maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam.
Waziri alikipongeza chuo hicho kwa maendeleo kilichofikia na kusaidia kutoa wataalamu
katika Nyanja za uhasibu na utunzaji wa hesabu ambapo sasa kinaendelea kupanua
huduma zake kwenye maeneo mengine nje ya makao makuu yake jijini Arusha.
Akimpatia maelzo waziri mpango, Afisa Uhusiano na Masoko wa
chuo hicho, Bi.Sarah Goroi, alimueleza Waziri Mpango kuwa chuo hicho kwa sasa
ukiacha makao makuu yake jijini Arusha pia kina matawi jijini Dar es Salaam,
jijini Mwanza na wilayani Babati mkoa wa Manyara.
Bi Goroi alisema, chuo kinatoa elimu ya uhasibu ngazi ya Astashahada(certificate),
Stashahada(Diploma), Shahada ya Kwanza(Bachelor degree), Post Graduate diploma,
na Shahada ya Uzamili (Masters Degree).
“Mheshimiwa waziri huduma tunazozitoa kwenye banda letu ni
pamoja na kufanya udahili hapa hapa kwa wanafunzi wanaotaka kujiunga na programu
mbalimbali zinazotolewa na chuo cheti kwa ngazi nilizozitaja.” Alifafanua Bi. Goroi
Alisema
Mtu anayehitaji kujiunga na chuo hicho, afike kwenye banda la chuo
akiwa na picha moja ya passport size ya rangi, na vivuli vya vyeti vya
kidato cha nne, (Form Four), na Kidato cha Sita,(Form Six), kwa wale
wanaoomba kujiunga na programu za Shahada ya Kwanza, au Cheti cha
kuhitimu elimu ya Chuo Kikuu kwa wale wanaotaka kujiunga na programu za
Masters.
Akieleza
zaidi Bi. Goroi alisema, kwa wanafunzi wanaotaka kujiunga na programu
za Astashahada (Cheti) wanapaswa wafike na vivuli vya vyeti vya
kumaliza elimu ya sekondari (Kidato cha nne)
Chuo cha Uhasibu Arusha, ni taasisi ya kielimu iliyoanzishwa
na sheria ya taasisi za elimu ya uhasibu Arusha ya mwaka 1990 (Act of 1990),
udhibiti wa jumla na uongozi wa taasisi uko chini ya Baraza la Uongozi la chuo,
(Governing Council), alifafanua Bi Goroi.
Waziri Dkt. Mpango, akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea banda hilo.
Katibu
wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, (NEC), anayeshughulikia masuala ya
Siasa na Uhusinao wa Kimataifa, Kanali (mstaafu), Nelubinga, (kulia),
akizungumza jambo wakati alipotembelea banda hilo, huku Afisa Uhusiano na Masoko wa
chuo hicho, Bi.Sarah Goroi(kushoto), akimsikiliza. Katikati ni Kanali Mstaafu, F.L Kakiziba.
Waziri
Dkt. Mpango, akifurahia jambo wakati akipatiwa maeelzo kuhusu huduma za
kielimu zitolewazo na Chuo hicho. Kulia ni Bi. Goroi
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, (NEC),
anayeshughulikia masuala ya Siasa na Uhusinao wa Kimataifa, Kanali
(mstaafu), Nelubinga, (katikati), akizungumza jambo wakati alipotembelea
banda hilo, huku Afisa Uhusiano na Masoko wa
chuo hicho, Bi.Sarah Goroi(kukulia), akimsikiliza. Kushoto ni Kanali Mstaafu, F.L Kakiziba.![]() |
Dkt.
Mpango, (kushoto), akisaini kitabu cha wageni kwenye banda hilo,
wanaoshuhudia kutoka kulia ni Afisa Utawala wa chuo Bi. Sekunda Titus,
Afisa Uadahili, Bw.Gerald Malisa, na Afisa Uhusiano na Masoko, Bi. Sarah
Goroi. Afisa Uhusiano na Masoko, Bi. Sarah Goroi, akimpatia maeelzo mama huyu. |













No comments :
Post a Comment