Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia
Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kukuza
matumizi ya teknolojia ya simu ili kufikia maendeleo endelevu
ulioandaliwa GSMA Mobile 360 Africa kwenye ukumbi wa Kimataifa wa
Mikutano wa Julius Nyerere. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
![]() | ||
| NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amesema Serikali itaendelea
kusimamia na kuweka mazingira bora yatakayosaidia mamia ya wananchi
nchini wanapata huduma za mawasiliano ya simu kwa njia ya kisasa zaidi
mjini na vijijini.
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu
Hassan ametoa kauli hiyo wakati anafungua Mkutano wa mwaka wa Chama cha
Makampuni ya Simu Duniani (GSMA MOBILE 360) Jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu
Hassana amesema anaimani kuwa wadau hao wa makampuni ya simu watajadili
kwa kina namna bora ya kufikisha mawasiliano ya kisasa kwa wananchi na
kuweka mipango mizuri ya kufikia wananchi wengi zaidi hasa maeneo
vijijini ambayo baadhi ya maeneo hayafikiki kutokana na uduni wa
miundombinu.
“Ningependa kusema kwamba
Tanzania inakubali sana ushirikiano na GSMA na tunatamani kupanua
ushirikiano wetu na uwezeshaji kwa Watu wetu kwa njia ya sekta ya simu
ili kufikia utekelezaji wa ajenda za Maendeleo endelevu ya Umoja wa
Afrika AU na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa 2020”.Amesisitiza Makamu wa
Rais.
Ameleeza kuwa kwa sasa Tanzania
ni miongoni mwa nchi kadhaa Kusini mwa Bara la Afrika ambayo inafanya
vizuri kwa wananchi wake kutuma fedha kwa kutumia simu za mkononi na
kusema kuwa hilo ni jambo zuri hasa kutokana na baadhi ya wananchi
kutokuwa na akaunti za benki hivyo huduma hiyo huwasaidia kwa kiasi
kikubwa kwa kutuma fedha kwa urahisi.
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu
Hassan amesisitiza umuhimu wa kuimarishwa zaidi kwa huduma za kisasa za
kimtandao ili wananchi waweze kunufaika zaidi kwa njia hiyo katika sekta
za elimu,afya, kilimo, biashara na masuala ya kijinsia.
Amewahakikishia wadau hao wa
makampuni ya simu kuwa Serikali ya awamu ya Tano itaendelea kushirikiana
nao bega kwa bega ili kuhakikisha sekta hiyo inaimarisha huduma zake
kwa njia ya kisasa kwa wananchi.
Makamu wa Rais amesema kuwa
Serikali ya itaendelea kujifunza kutoka nchi zingine ambazo zimefanya
vizuri katika sekta ya mawasiliano ili taifa na wananchi wake liweze
kunufaika ipasavyo na huduma hizo kwa ajili ya maendeleo endelevu.
Kwa upande wake, Waziri wa
Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mbarawa amesema
akizungumza katika mkutano huo ameeleza kuwa Serikali itaendelea
kushirikiana kwa karibu na Makampuni ya Mawasiliano ili kuhakikisha
huduma zinazotolewa kwa wananchi zinakuwa na ubora unaotakiwa.
|
Baadhi ya Wageni waalikwa mbalimbali wakimsikiliza Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
alipokuwa akihutubia wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kukuza matumizi ya
teknolojia ya simu ili kufikia maendeleo endelevu ulioandaliwa GSMA
Mobile 360 Africa kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius
Nyerere. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)


No comments :
Post a Comment