Monday, July 31, 2017

KIFUA KIKUU BADO NI TATIZO KUBWA KWENYE MAENEO YA MACHIMBO


 Meneja Mpango wa Taifa wa kudhibiti
kifua kikuu na  ukoma Dr,Beatrice Mutayoba Akielezea hali ilivyo ya
maambukizi ya kifua kikuu kwenye maeneo ya migodini wakati wa kikao ambacho
kiliwakitanisha wadau wa sekta ya afya pamoja na wadau wa sekta ya uchimbaji
madini.
Wajumbe wakifuatilia hotuba ya Meneja Mpango wa Taifa wa kudhibiti kifua kikuu na  ukoma Dr,Beatrice Mutayoba wakati wa kikao hicho
Mwakilishi wa mganga mfawidhi wa hospital ya
Mkoa  huo ambaye pia ni katibu,Sashisha
mafuwe akielezea tatizo la kifua kikuu ambavyo lilivyo kwenye mkoa wa Geita.
 
Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa  Huo ambaye pia ni Msaidizi wa katibu Tawala
Mkoani Humo.Emmily Kasagara  akiwataka wajumbe kutumia kikao hicho kujadili namna ambavyo wataweza kupambana na ugonjwa huo
Imebainika kuwa maeneo ambayo kunafanyika shughuli za uchimbaji bado kuna tatizo kubwa la
maambukizi ya ugonjwa wa kifua kikuu ni kutokana na kuwepo kwa msongamano
mkubwa wa watu ambao wanafanya shughuli hizo.
 
Hayo yamebainishwa na Meneja Mpango wa Taifa wa kudhibiti kifua kikuu na  ukoma Dr,Beatrice Mutayoba wakati wa kikao ambacho kimewakutanisha wadau mbali mbali wakiwemo wa sekta ya afya na madini Mkoani Geita.
 
Amesema kuwa pamoja na tatizo la kifua kikuu kuwa juu bado kunatatizo kubwa la uelewa kwa
watu wanaishi kwenye machimbo pamoja na wahudumu wa afya  ambao wapo kwenye maeneo hayo.
 
“Pamoja na jitihada ambazo zinaendelea lakini bado tunaona changamoto kubwa ni elimu
tumefika kijiji kimoja tukamuuliza muhudumu wa afya je unaelewa dalili za kifua
kikuu anasema dalili moja wapo ni mtu kutokwa na mkojo mwingi hivyo tumeona
sisi ni tatizo kubwa sana”Alisema Mutayoba.
 
Aidha  mwakilishi wa mganga mfawidhi wa hospital ya Mkoa  huo ambaye pia ni katibu,Sashisha
mafuwe ameeleza kuwa  kati ya maeneo ambayo yanaweza kupewa kipa umbele kwenye shughuli hiyo ya uelimishaji ni pamoja na Mkoa huo kutokana na shughuli ambazo zimekuwa zikifanyika  za uchimbaji.
 
Kwa upande wao wadau ambao wanashirkiana na serikali kwenye mapambani ya kifua  Dr,Kiva mvungi ambaye ni mganga mkuu wa mgodi wa GGM ameelezea kuwa wao ni moja kati ya watu ambao wameendelea kupambana na kifua kikuu kwa kuboresha maeneo ya kufanyia kazi hususani kwa wafanyakazi.
 
Bi,Ena Lutenga ambaye anatokea shirika la umoja wa mataifa la wahamaji  pia ameongeza wao wanashiriki katika kuweka mazingira safi ya wakimbizi na kutokomeza ugonjwa huo kwenye maeneo ambayo ni ya wakimbizi.
Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa  Huo ambaye pia ni Msaidizi wa katibu Tawala Mkoani Humo.Emmily Kasagara ,ameishukuru wizara ya afya kupitia mpango wa kutokomeza ugonjwa wa kifua kikuu kuchagua Mkoa huo katika utoaji wa elimu.
 

No comments :

Post a Comment