Monday, July 31, 2017

MAGARI 40 YANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI TABORA KUFUATIA MSAKO ULIOFANYWA NA MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BIMA (TIRA) KANDA YA KATI, WA KUBAINI VYOMBO VYA MOTO VYENYE BIMA FEKI.


Meneja
wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima nchini  Kanda ya Kati
Bi.Stella Rutaguza akizungumza na madereva pamoja na
makondakta katika stendi kuu ya mabasi mkoani Tabora ,walipokwenda
kugagua bima za vyombo vya moto kama ni halali ama feki.Picha na Vero
Ignatus Blog

 
 Afisa Mwandamizi wa Bima Maneno Adam kutoka Mamlaka
ya Usimamizi wa Bima( TIRA)akikagua gari ili kuangalia kama bima
inayotumika kama ni halali ama ni feki .Picha na Vero Ignatus
Blog.

  Ukaguzi wa magari ukiendelea katika stendi kuu ya
mabasi Mkoani Tabora kama inavyoonekana kwenye picha kutoka kushoto ni
Meneja wa Kanda ya kati kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bima nchini
bi.Stella Rutaguza akiwa na askari wa kikosi cha usalama barabarani
Koplo Clement   .Picha na Vero Ignatus Blog.
Zoezi
la ukaguzi likiendelea wakati huohuo madereva ,makondakta pamoja na
abiria wakipata elimu namna ya kutambua Bima kama ni halali ama
feki.Picha na Vero Ignatus Blog.


 
Wananchi ,madereva ,makondakta wa mabasi makubwa na
madogo wakipewa elimu na namna ya kut5ambua bima feki kwa
kutumia  simu ya mkononi au kwa njia ya mtandao mfumo wa TIRA MIS
.Picha na Vero Ignatus Blog.


Na   Vero Ignatus,
Tabora
Mamlaka
ya usimamizi wa Bima nchini (TIRA) imefanya zoezi la ukaguzi wa
bima za vyombo vya moto katika manispaaa ya Tabora katika stendi kuu
ya mabasi na kubaini magari mengi hayana bima na mengine yana bima
tofauti na kile kilichoorodheshwa katika bima hizo.
Akizungumza juu ya zoezi hilo meneja ( TIRA) Kanda ya Kati Stella
Rutaguza
amesema kuwa katika wameweza kukagua magari zaidi
ya 266 magari 27 yamebainika kuwa na bima za kughushi
,magari 13 hayakuwa na bima,magari mengine yanatumia bima za
pikipiki,na baadhi ya magari madogo yanatumia bima za magari ya
mizigo.
“Magari
tuliyoyakagua na kuyakuta yana bima feki tumeyakamata na kuyapeleka
kituoni ili kwamba watupe maelezo  kuwa hizo bima wamezipata
wapi,”alisema
Amesema kwa ada za malipo ya bima kwa mujibu wa sheria kwa
maana ya bima ndogo (Third party insurance) kwa jumla magari haya
40 ni shilingi Milioni  33,850,000/= ambapo magari
hayo yaliyokamatwa ni mabasi ya abiria 65,Coster za abiria 26, Noa na
magari madogo ya binafsi.
 Imebainika kuwa kuna wamiliki wa magari ambao
walikuwa wamenunua bima kubwa (Comprehensive Insurance) ambapo kwa
mabasi walikuwa wamelipia kuanzia shs.3,000,000/= na zaidi
ambazo zimeingia kwenye mifuko ya matapeli wa bima.
“Tunataka
hawa vishoka wa bima feki watafute kazi nyingine  halali za
kufanya  kwani Mamlaka ya usimamizi wa Bima nchini haitawafumbia
macho wadanyanyifu hawa
Bi Stella
amesema kuwa kesi za matapeli wa bima zimekuwa zikikaa muda mrefu bila
kupekekwa mahakamani na hata zikipelekwa zimekuwa zikichukua  pia
muda mrefu pia.
‘Tunaomba
kesi za Bima ziwe zinashughulikiwa kwa haraka na mamlaka husika
“alisisitiza bi Stella. 
Meneja huyo wa kanda ya kati Stella ametoa
rai kwa mawakala wa bima na kusema kuwa yeyote atakayegunduliwa anauza
bima feki atakamatwa na kupelekwa kwenye vyombo vya sheria na
atafutiwa leseni  maana amekiuka taratibu za kisheria
.
” Hawa
watu wengi wanaouza hizo feki bima siyo wakala wa bima ila ni matepeli
tu wamtaani hivyo tukiwabaini tutawapeleka kwenye vyombo vya sheria
hatuna utani wala mchezo katika hili”.alisema.
 ********************************************************
Namna
ya KUHAKIKI BIMA Kama ni  HALALI ama feki

 
Kwa njia
ya simu ya mkononi  nenda kwenye uwanja wa ujumbe
mfupi  andika neno STIKA weka namba ya stika tuma
kwenda namba 15200

Kwa
kupitia njia ya mtandaoni (internet)kwenda kwenye tovuti ya Tira
mis  

htt/mis.tira.go.tz kisha ingiza namba za stika na
bofya hakiki.

No comments :

Post a Comment