Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (Wa pili kushoto)
akitoa maelekezo kwa Mkandarasi anayejenga Kituo cha Mzani cha Singiwe Kilichopo
katika barabara ya Sumbawanga-Matai-Kasanga Port (112KM) Mkoani Rukwa wakati alipokagua ujenzi huo Mkoani Rukwa.
NA WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO.
SERIKALI
kupitia Wakala wa barabara nchini TANROADS mkoa wa Rukwa imekamilisha
ahadi yake kwa wananchi ya kuwapunguzia changamoto ya usafirishaji wa abiria na
mzigio kwa kukamilisha ujenzi wa Daraja la mto Kalambo pamoja na barabara ya Sumbawanga Matai hadi Kasanga
port (112km) ambapo Kilomita 71.4 zimeshawekwa lami.
Akizungumza
mara baada ya kukagua daraja na barabara hiyo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Eng. Edwin Ngonyani amesema kukamilika kwa barabara hiyo kutafungua fursa za kiuchumi
kwa wananchi wa mkoa Rukwa na nchi nyingine za jirani ikiwemo Jamhuri ya
kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Burundi.
"Tuliwaahidi
wananchi kujenga darala na barabara hii
ili wafanyabiashara na wakulima waweze kusafirisha bidhaa na mazao yao kwenda
katika masoko kwa wakati na hivyo kukuza uchumi wao binafsi na taifa kwa
ujumla,” ameaema Eng. Ngonyani.
Ameongeza
kuwa chini ya uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli Serikali itahakikisha ndani
ya kipindi cha miaka mitano inakamilisha ahadi zote walizoahidi kwa wananchi
ili wananchi wanufaike na Serikali yao.
"Serikali
ya Dkt. John Pombe Magufuli ipo kwa ajili ya wananchi wote, na sisi kama
wasimamizi tuliopewa dhamana kwenye Wizara tutahakikisha kile tulichokiahidi
kwa wananchi tunakitekeleza kwa wakati ili wananchi wanufaike na uchumi
wa nchi ukue,” amesisitiza Eng. Ngonyani.
Kwa
upande wake Meneja wa Tanroads Rukwa amewataka wananchi kutunza miundombinu ya
barabara na kuacha vitendo vya kung'oa alama za barabarani ambazo zimewekwa ili
kuongeza usalama kwa madereva katika matumizi ya barabara hizo.
"Tumeweka
alama hizi barabarani kwa ajili ya kuongoza madereva wanaotumia barabara ili
kuepusha ajali zinazoweza kutokea kwa kutokuwepo na alama za tahadhari, hivyo ni
wajibu wenu kuzilinda na kuzitunza kwani zipo kwa faida yetu sote,” amesema Eng.
Msuka Mkina
Katika
hatua nyingine Waziri Ngonyani amekagua huduma za bandari ya Katanga ambapo
amesema Serikali itaendelea kuziboresha bandari zilizopo ukanda wa ziwa
Tanganyika ili kuvutia wasafirishaji wa mizigo mikubwa kutumia bandari hizo.
"Tutaendelea
kuimarisha miundombinu ya bandari ya Kalema, Kigoma na Katanga ili ziwe na
uwezo wa kupakia na kupakua mizigo mikubwa kwenda Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo (DRC) na Burundi,” amesisitiza Eng. Ngonyani.
Naye
Msimamizi wa Bandari Mkoa wa kigoma, Bw. Morris Mchindiuza amesema Mamlaka ya
bandari TPA imejipanga na imetenga kwenye bajeti yake kiasi cha Sh. bilioni 1
kwa ajili ya upanuzi wa Gati namba moja
na hivyo kuchochoa ukuaji wa wa kibiashara na ongezeko la Meli hususani nchi za
jirani kama Burundi na DRC Congo.
Naibu
Waziri Eng. Ngonyani yupo katika Ziara ya kukagua Miundombinu ya barabara,
Viwanja vya Ndege, Ujenzi wa Nyumba za viongozi, huduma za mawasiliano ya simu,
Bandari na Madaraja katika Mkoa wa
Rukwa
Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (Wa pili kulia)
akipokea taarifa ya ujenzi ya barabara ya Sumbawanga-Matai-Kasnga Port (112KM)
Mkoani Rukwa wakati alipokagua ujenzi
huo Mkoani Rukwa.
Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (Wa pili)
akielekeza jambo kwa Msimamizi wa bandari ya Kigoma,Bw. Morris Mchindiuza (Wa
kwanza) wakati alipokagua huduma za bandari ya Katanga Mkoani Rukwa.
Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (aliyenyoosha
kidole) akiongea na wakazi wa kijiji cha Katete Wilaya ya Sumbawanga Mkoani
Rukwa wakati alipokagua barabara ya Matei-Kasesya (KM).
No comments :
Post a Comment