Wednesday, July 12, 2017

CONOR MCGREGOR ATISHIA KUMDUNDA KWA KO FLOYD MAYWEATHER

Mpiganaji Conor McGregor anayepigiwa chapuo la kushinda pambano amempiga mkwara bondia Floyd Mayweather kuwa atamdunda kwa KO wakati wakiwa katika ziara ya dunia ya kupromoti pambano lao Jijini Los Angeles.

Mbele ya mashabiki elfu 11 katika ukumbi wa LA's Staples Center, Mayweather na McGregor walikutana uso kwa uso kwa mara ya kwanza tangu kuthibitishwa rasmi kwa pambano lao hilo litakalowajaza mkwanja mrefu.

Licha ya Mayweather kuwa katika ukumbi wa nyumbani akiwa amevalia traksuti yenye nyota, bondia huyo Mmarekani alijikuta akizomewa na mashabiki wake, huku idadi kubwa ya watu wakimshangilia McGregor.
                                       Conor McGregor akimchimbia mkwara Floyd Mayweather
                             Floyd Mayweather na Conor McGregor wakizuiwa wasizidunde

No comments :

Post a Comment