Huawei kampuni
ambayo inaoongoza kwenye Teknolojia ya Mawasiliano (ICT)
duniani, imesema ipo tayari kufanya kazi na serikali za Afrika na
taasisi binasfi ili kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa Bara la
Afrika kupitia kuhimiza mfumo wa...
mawasiliano ya mobile broadband, ambapo
wametangaza simu ya GSMA 360 kwa Afrika wakianza na Dar es Salaam leo.
Huawei imeonyesha dhamira yake ya
kuboresha jamii kwa kushirikiana na wadau wengine kusaidia kuongeza
wigo wa matumizi ya matandao na kuanzisha simu za mezani za nyumbani za
wireless ambazo zitatuma mfumo wa mawasiliano wa simu za mkononi (MBB)
jambo ambalo litaogeza matumizi ya kidijitaji katika maeneo ya mjini na
vijijni.
Kupanua wigo wa matumizi ya MBB
maeneo ya nchi mbalimbali za barani Afrika itasaidia kupunguza umaskini
na kuimarisha huduma za afya na elimu pamoja na kupanuna wigo wa
kuimarika kifedha.
GSMA inakadiria kwamba baada ya
miaka mitano iajyo kutakuwa na takribani simu milioni 720 za smartphone
ambazo zitakuwa zinatumika na asilimia 60 ya mfumo wa MBB utakuwa
umeunganishwa kwenye soko la Afrika.
Kuunganishwa kwa mfumo huo kutaongeza ushindani kwenye nchi, pia ubunifu na kuongezeka kwa uzalishaji.
Changamoto kubwa katika viwanda
vinakabiliwa na uwezo wa kujitanua katika maeneo ya mijini na vijiji
inajumuisha suala la ugumu wa upatikanaji wa maeneo, gharama za juu za
miundombinu na kutorudi kwa mitaji yao wanayowekeza.
Kutokana na kuwapo vikwazo hivyo
kwa ukuaji wa maendeleo, Huawei imedhamiria kusaidiana na wadau
jkupitia kupunguza gharama za uendeshaji, kwa kuamua kuwekeza kupitia
kuimarisha mawasiliano.
Huawei imekuja na njia tatu za
kukabiliana na hali hiyo ambazo niu PoleStar, TubeStar na
RuralStar. Njia hizi tatu zitasaidia kuleta suluhisho ambapo italeta
urahisi na gharama nafuu.
Makamu wa Rais wa Huawei,
anayeshughulikia masuala ya Wireless Networks Marketing na ambaye pia ni
Mkuu wa Kitengo cha Global Demand Generation, Dk Mohamed Madkour
alisema dhamira ya Huawei ni kukuza maendeleo ya kijamii na uchumi kwa
Afrika kupitia mawasiliano.
Dar Mohamed Madkour alisema,
“Licha ya kuanzisha huduma ya mtandao katika mataifa mbalimbali Afrika,
pia tunafanya biashara tatu na kuendeleza viwanda. Jambo la kwanza ni
mifumo ya simu kwa mfano video cloud, game cloud a music cloud. Pili
uunganishaji wa mifumo viwandani na tatu ni uunganishaji mifumo ya
nyumbani.
Ongezeko la matumizi ya mitandao
ya simu imefungua mlango kuimarika kwa biashara ya matumizi ya simu na
mitandao ambapo kumekuwapo na 4G, 4.5G na nyingine ya 5G inakuja.
“Tumekuwa mstari wa mbele katika
kuangalia fursa za Afrika licha ya changamoto zote ambazo
tumezibainisha. Huduma ya mawasiliano inahitaji kuonyeshwa vitendo na
kuanzisha biashara inayofaa ili kuzitumia fursa zote,” alisema Mohamed.
No comments :
Post a Comment