Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha ( RPC ), Charles Mkumbo amesema
wanamshikilia mmiliki wa basi dogo aina ya Coaster ambayo ilipata ajali
na kusababisha vifo kwa wanafunzi, walimu na dereva wa shule ya Lucky
Vincent iliyoko Kwa-Mrombo kata ya Olasiti jijini Arusha
Kamanda
Mkumboamesema pia Polisi inamshikilia mmiliki wa shule hiyo kwa
kuruhusu gari yake hiyo kubeba abiria wengi zaidi kuliko uwezo wake.
"Siku ya tukio walikuwepo abiria 38 kwenye gari katika uchunguzi baada
ya kubaini hilo tumeshachukua hatua kwa mtu aliyewezesha gari hilo
kupakia hao watu, tumeshamkamata mmiliki wa gari ambaye ndiye mwenye
shule hii, sasa hivi tunaendelea na uchunguzi na utakapokamilika
atafikishwa mahakamani" alisema RPC wa Arusha.
Kwa mujibu wa Mkumbo anasema gari hiyo ilikuwa na kibali cha kubeba watu 30 lakini siku ya ajali ilikuwa na watu zaidi ya 30.
Aliekuwa
Mkuu wa wilaya ya Lindi, Yahaya Nawanda, (katikati), akikata utepe kuzindua
mradi wa”Hakuna wasichoweza”
unaowapatia elimu ya hedhi na vifaa vya kujistiri wasichana ili wasikose
kuhudhuria masomo yao mashuleni, Mradi huo unadhaminiwa na Vodacom Tanzania Foundation
na kuendeshwa na T-Marc Tanzania mkoani humo,Wengine katika picha kutoka
kushoto ni Aisha Mahadni mwanafunzi wa shule ya msingi stadium,Renatus
Rwehikiza aliekuwa mkuu wa Vodacom Tanzania Foundation,Mkurugenzi wa T-Marc
Tanzania,Diana Kisaka na Lalat Saidi.
No comments :
Post a Comment