Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab
Telack akizungumza na ujumbe alioambatana nao akiwa katika shamba la
mtama kijiji cha Busongo kata ya Mwamashele. Wengine pichani katikati ni
Mkuu wa wilaya hiyo, Nyabaganga Taraba na Ofisa Kilimo, Umwagiliaji na
Ushirika, George Kessy.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu,
Nyabaganga Taraba akimuonesha Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack
maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya fursa za uwekezaji viwanda eneo la
Uchunga. Wengine pichani kulia ni Katibu Tawala Wilaya, Shadrack
Kangese, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya wilaya hiyo, Mang’era
Mang’era
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab
Telack (kulia) na Mkuu wa wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Taraba
wakiangalia namna mzani wa kupimia choroko unavyofana kazi katika eneo
la Mhunze.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab
Telack akizungumza ndani ya kiwanda kidogo cha kutengeneza bidhaa za
ngozi zikiwemo viatu wakati wa ziara hiyo.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab
Telack akizungumza na baadhi ya wafanyabishara akiwa katika eneo la
Mhunze wakati wa ziara hiyo.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack akiangalia viatu vilivyotengenezwa na kikundi cha Badimi wakati wa ziara hiyo.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab
Telack amefanya ziara katika wilaya ya Kishapu na kutembelea na kukagua
maeneo yenye fursa mbalimbali za uwekezaji viwanda.
Katika ziara hiyo Telack aliweza
kutembelea vikundi vya wananchi wanaotengeneza bidhaa za ngozi, mbunifu
wa mashine za kukoboa nafaka na wakulima wa zao la mtama kata ya
Mwamashele.
Akiwa katika kata ya Kishapu eneo
la Mhunze alitembelea wanakikundi cha Badimi na kujionea bidhaa
mbalimbali za ngozi zikiwemo viatu kuwataka Watanzania kupenda bidhaa za
nchini.
Akiwa ameambatana na mwenyeji wake
Mkuu wa wilaya hiyo, Nyabaganga Taraba pamoja na viongozi mbalimbali
alisifu jitiada za kikundi hicho huku akiwataka Watanzania kupenda
bidhaa za ndani.
Kwa upande wao vijana hao
walimhakikishia kuwa wanaweza kutengeneza viatu kw ajili ya mkoa mzima
lakini wanakabiliwa na changamoto ya uhaba wa malighafi na mashine.
Mkuu wa wilaya, Taraba alisema
halmashauri hiyo iko nao bega kwa bega na tayari imetenga fedha kiasi
cha sh. milioni 18 katika mwaka ujao wa fedha ili kukisaidia kikundi
hicho.
Katika ziara hiyo pia mkuu huyo wa
mkoa alimtembelea mwananchi Daudi Nkende ambaye mbunifu wa mashine za
kukoboa nafaka zikiwemo mtama katika eneo la Uchunga.
Telack alisema kuwa Serikali
imefungua milango kwa wabunifu wa vitu mbalimbali na hivyo washiriki ili
kuunga mkono jitihada zake katika kutekeleza Sera ya Viwanda.
No comments :
Post a Comment