Wanafunzi wa Shule ya Msingi
Kyakairabwa wakimsikiliza Afisa Mahusiano na Masoko Mkuu wa TADB, Bw.
Saidi Mkabakuli wakati walipotembelea Banda la TADB ili kujua shughuli
za Benki hiyo kwenye Viwanja vya Kyaikarabwa yanapofanyika Maadhimisho
ya Wiki ya Maziwa mkoani Kagera.
Wanafunzi wakifuatilia machapisho
mbalimbali kuhusiana na Benki ya Kilimo katika Banda la TADB katika
Viwanja vya Kyakairabwa mjini Bukoba wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya
Maziwa yanayoendelea mjini humo.
Shindano la kujua Shughuli za TADB
kwa Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kyakairabwa wakifuatilia kwa makini
machapisho ili waweze kujishindia zawadi kutoka TADB.
Mshindi wa Tatu wa Shindano la
kujua Shughuli za TADB, Gidion Geoffrey (12) mwanafuzi wa Darasa la Tano
wa Shule ya Msingi Kyakairabwa akikabidhiwa Zawadi yake. Gidion alijibu
kuhusu Majukumu ya Benki ya Kilimo.
Mshindi wa Pili wa Shindano la
kujua Shughuli za TADB, Delphina Geoffrey (11) mwanafuzi wa Darasa la
Nne wa Shule ya Msingi Kyakairabwa akikabidhiwa Zawadi yake. Delphina
alijibu Kuhusu Mikopo inayotolewa na TADB.
Mshindi wa Kwanza wa Shindano la
kujua Shughuli za TADB, Anna Julius (9) mwanafuzi wa Darasa la Tatu wa
Shule ya Msingi Kyakairabwa akikabidhiwa Zawadi yake. Anna alijibu
kiuweledi mkubwa shughuli za Benki na Kaulimbiu yake licha ya umri wake
mdogo.
………………………..
Katika kuadhimisha Wiki ya Maziwa
inayofanyika mjini Bukoba, wanafunzi wa Shule ya Msingi Kyakairabwa
walijitokeza kwa wingi katika Banda Benki ya Maendeleo ya Kilimo
Tanzania (TADB) ili kujua shughuli za Benki hiyo kwenye Viwanja vya
Kyaikarabwa.
Wanafunzi hao walipata fursa ya kujifunza shughuli na huduma zinazotolewa na Benki hiyo.
Akizungumza na wanafunzi hao,
Afisa Mahusiano na Masoko Mkuu wa TADB, Bw. Saidi Mkabakuli aliwajulisha
wanafunzi hao kuwa TADB ni Taasisi ya Serikali iliyo chini ya Msajili
wa Hazina na ilianzishwa kwa madhumuni makubwa mawili ambayo ni
kusaidia upatikanaji wa utoshelezi na usalama wa chakula ambao ni
endelevu nchini Tanzania; na kuchagiza na kusaidia Mapinduzi ya Kilimo
kutoka kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye
ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini nchini.
Bw. Mkabakuli aliwaeleza kuwa
Serikali iliambua kuianzisha Benki hiyo ili kutatua changamoto za ufinyu
mkubwa wa upatikanaji wa fedha mikopo kwa ajili ya maendeleo ya kilimo
nchini ambao unachangiwa kwa kiasi kikubwa na mikopo mingi kutoka
taasisi za fedha kuelekezwa zaidi kwenye upande wa biashara za bidhaa.
Aliwatajia changamoto nyingine
zilizopelekea Serikali kuianzisha TADB kuwa ni pamoja na riba kubwa
kwenye mikopo ya kilimo; mikopo ya muda mfupi; masharti magumu ya kukopa
bila kuzingatia hali halisi ya sekta ya kilimo na mazao ambayo
inaathiriwa kwa kiasi kikubwa na mabadiliko ya hali ya hewa.
“Kutokana na changamoto hizo,
Serikali iliamua kuanzisha Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB)
ili kusaidia kukabiliana na mapungufu hayo na kuhuisha upatikanaji wa
mikopo katika sekta ya kilimo ili kuleta mapinduzi katika kilimo
nchini,” Bw. Mkabakuli aliwaeleza wanafunzi hao.
Katika kuwapima uelewa wao,
wanafunzi hao walishindanishwa Shindano la kujua Shughuli za TADB na
washindi walipatiwa zawadi mbalimbali.
No comments :
Post a Comment