Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Yamungu Kayandabila akiongea na
watumishi wa wizara hiyo katika mkutano wa Baraza la Wafanyakazi na
kuwataka waongeze jitihada za makusanyo ya kodi ya pango la ardhi.
Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakimsikiliza kwa makini Katibu
Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Yamungu Kayandabila wakati wa mkutano wa Baraza
la Wafanyakazi.

Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Yamungu Kayandabila katikati, Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Dkt. Moses Kusiruka kushoto na Mjumbe Baraza
kuu la Wafanyakazi Serikalini (TUGHE) kulia, wakiimba wimbo wa
mshikamano kwa wafanyakazi.

Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakiimba wimbo wa mshikamano kwa
wafanyakazi wakati wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi.
Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakiimba wimbo wa mshikamano kwa
wafanyakazi wakati wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi.
………………………………………………………
Na. Hassan Mabuye, Kitengo cha Mawasiliano, Wizara ya Ardhi.
Serikali imefanikiwa kukusanya
jumla ya kiasi cha shilingi bilioni 76 cha makusanyo ya kodi ya pango la
ardhi hadi kufikia tarehe 13 Mei 2017 kiwango ambacho hakijawahi
kufikiwa.
Akiongea katika mkutano wa Baraza
la Wafanyakazi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Yamungu Kayandabila amesema kiwango cha
makusanyo ya kodi ya ardhi hakijawahi kufukiwa ukilinganisha na miaka ya
nyuma ambapo kwa sasa Wizara ya Ardhi imeisha kusanya kiasi cha
shilingi bilioni 76 cha kodi ya pango la ardhi.
Juhudi za kukusanya kodi ya pango
la ardhi kwa viwanja vilivyopimwa zinaendelea vizuri licha ya
changamoto iliyopo hususan muamko wa wananchi katika kulipa kodi,
amesema Dkt. Kayandabila.
“Ni matumaini yangu kuwa katika
kipindi kilichobaki Wizara itafikia lengo la kukusanya kiasi cha
makusanyo ya kodi ya pango la ardhi kilichowekwa kwa mwaka wa fedha
2016/2017 ambacho ni kiasi cha shilingi bilioni 111.7”. Amesema Dkt.
Kayandabila.
Amesema, Serikali kuanzia mwezi
julai, 2017 kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
itaanza kukusanya kodi ya pango la ardhi kwenye viwanja na mashamba
yasiyopimwa. Lengo la utaratibu huu ni kuongeza wigo wa mapato
yatokanayo na kodi ya pango la ardhi.
Utaratibu huu utawafanya wananchi
wote wanaomiliki ardhi waweze kulipa kodi. Hata hivyo, ni vema ieleweke
kuwa uamuzi huu hauna lengo ya kupunguza juhudi za Wizara katika
kupanga, kupima na kumilikisha ardhi kwa wananchi, isipokuwa utaratibu
huu unajenga dhana ya uwajibikaji kwa wananchi wote katika kulipa pango
la ardhi kwenye maeneo yao.
Aidha, serikali imeanza Ujenzi wa
mfumo wa kielektronic wa kumbukumbu za Ardhi (Integrated Land
Management System) ambao umeanza kutekelezwa. Mfumo huo ukikamilika
utasaidia sana kuwa na kumbukumbu sahihi za wamiliki wa ardhi na hivyo
kurahisisha ukusanyaji wa kodi za Ardhi.
No comments :
Post a Comment