Treni
ya abiria iliyokuwa ikitokea jijini Dar es salaam kwenda Mikoa ya
Tabora, Mwanza na Kigoma, imepata ajali usiku wa kuamkia leo Mei 13, 2017 katika eneo
la stesheni ya Mazimbu Mkoani Morogoro.
Kwa
mujimu wa Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Reli Tanzani, Bw.
Midladjy Maez
amesema ajali hiyo imetokea majira ya saa tano usiku baada ya Mabehewa
matatu kuacha njia na mengine manne kuegama na kusababisha abiria mmoja
alietambulika kwa jina la Ashura Mrisho aliyekuwa akitokea Ngerengere
kwenda Tabora kujeruhiwa na baada ya kuangukiwa na mizigo.
Mabehewa
13 yamerejeshwa Morogoro ili kufanyika utaratibu wa kuwapangia usafiri
mbadala abiria wa treni hiyo. Taarifa zaidi zitafuata wakati Uongozi wa
TRL, Wahandisi na Mafundi wa reli wakishughulikia ajali hiyo.
Bw.Midladjy Maez |
No comments :
Post a Comment