Maofisa Waandamizi waliowakilisha TBL Group katika
mkutano huo (Kushoto) ni Lucy Manning -ABInBev Quality Assurance East
Africa, na Manoj Kr. Chaudary- ABInBev Energy, Fluid & Maintenance
Coordinator East Africa
Baadhi ya wawezeshaji katika mkutano huo wakitoa mada zinazohusiana na biashara ya viwanda
…………………………
Mkutano unaohusu uzalishaji viwandani na changamoto zinazokabili sekta ya viwanda katika kanda ya Afrika Mashariki umemelizika mjini Kigali na kushirikisha wawekezaji wa sekta ya viwanda kutoka nchi mbalimbali.
Miongoni mwa makampuni kutoka Tanzania ambayo yalishiriki katika mkutano huo ni TBL Group ikiwakilishwa na ujumbe kutoka kampuni yake mama ya ABInBev.
Katika
mkutano huo zilijadiliwa changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya
viwanda hususani katika maeneo ya masoko ya bidhaa kikanda,ushindani wa
kibiashara,na washiriki walibadilishana uzoefu na kuweka mikakati ya
kupambana na changamoto hizo.
Baadhi
ya changamoto ambazo zilionekana kuwa kubwa na kuzorotesha uwekezaji
katika sekta ya viwanda ni tofauti ya mazingira sawa ya uwekezaji hali
inayosababisha ubora na bei za bidhaa kuwa tofauti,uingizwaji
wa bidhaa feki kwenye masoko,kukithiri kwa biashara haramu ,
kutozingatia sheria ya hakimiliki kwa wazalishaji na jinsi ya
kubadilishana wataalamu baina ya nchi na nchi kutokana na sheria mgumu za kazi zilizopo .
Maazimio yaliyofikiwa katika mkutano huo baadhi yake ni kuondoa vikwazo
vinavyosababisha gharama za kuuza bidhaa kubwa kutokana na gharama
kubwa za uendeshaji na pia washiriki waliazimia kuzingatia kanuni za
kufanya uzalishaji usio na athari na mazingira.
Kwa upande wa Tanzania kampuni
ya TBL Group imeanza kuutekeleza kwa kufanya uzalishaji kwa kutumia
teknolojia ya nishati inayotokana na pumba za mpunga katika kiwanda
chake cha Mwanza na kutumia umeme wa nishati ya jua katika mchakato wa
uzalishaji katika kiwanda chake kilichopo mkoani Mbeya.
Mbali na matumizi ya nishati mbadala isiyo na athari kwa mazingira,kampuni ya TBL Group pia imefanikiwa kupunguza matumizi makubwa ya maji katika uzalishaji wa bia kutokana na kutumia teknolojia za kisasa.
No comments :
Post a Comment