Bw. Justine Ngaile Mkurugenzi wa
Kinga na Mionzi kutoka Tume ya Atomiki akiwasilisha mada kwa Naibu
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Luhaga Mpina. Waziri Mpini alikutana
na Taasisi zinazohusika na usimamizi wa kemikali kujadilili mkakati wa
pamoja wa kusimamia kemikali nchini.
Baadhi ya wataalamu kutoka Taasisi
ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Mamlaka ya Chakula na Dawa na Tume ya Nguvu
za Atomiki wakifuatilia majadiliano na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa
Rais-Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina (hayupo pichani), kikao
kazi hicho kimefanyika katika Ofisi ya Makamu wa Rais Dodoma.
……………..
Na Lulu Mussa,Dodoma
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu
wa Rais Muungano na Mazingira, hii leo amekutana na taasisi zizohusika
na uratibu na usimamizi wa kemikali hapa nchini.
Akiongea na Taasisi hizo, Waziri
Mpina amewaagiza watendaji hao kudhibiti na kusimamia kemikali hatarishi
nchini ikiwa ni pamoja na kuratibu usafirishaji, usambazaji na matumizi
ya
kemikali hizo hapa nchini kwa namna bora zaidi.
Waziri Mpina amezitaka taasisi
hizo kutoa taarifa za utendaji wa kazi kila robo ya mwaka kwa Baraza la
Taifa la Hifadhi na Usimizi wa Mazingira kwa mujibu wa Sheria ya
Mazingira kifungu namba 170. “Nawaagiza kuwasilisha takwimu za kemikali
zinazozalishwa nchini, zinazoagizwa au kusafirishwa nje ya nchi, pamoja
na kuainisha viwanda vinavyozalisha kemikali vilivyosajiliwa na maghala
yaliyosajiliwa kuhifadhi kemikali hizo” alisisitiza Mpina.
Katika kikao hicho Waziri Mpina
pia ameliagiza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira
nchini ndani ya miezi miwili kuandaa muongozo na kuupitisha katika hatua
zote wa namna bora ya kuteketeza taka hatarishi bila kuathiri
mazingira.
Aidha Waziri Mpina ameagiza
kuandaliwa kwa andiko litakalobainisha umuhimu wa kuteketeza taka
hatarishi. “Kama taifa ni lazima tuwe na “dedicated Incinerator” kubwa
kutekeza taka hizo hatarishi kwa kuzingatia taka zinazozalishwa hapa
nchini” Mpina alisisitiza.
Katika hatua nyingine, Baraza la
Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira nchini, Wakala wa Maabara ya
Veterinari Tanzania, Tume ya Nguvu za Atomiki, Taasisi ya Utafiti ya
Viuatilifu katika Kanda za Kitropiki, Mamlaka ya Chakula na Dawa, OSHA
na Mkemia Mkuu wa Serikali kwa pamoja wametakiwa kuanda Hati ya
Makubaliano ya kuratibu utekelezaji wa majukumu yao ikiwa ni pamoja na
kuhuisha Sheria zao na kuleta mapendekezo Serikali ya vifungu vya
kufanyiwa marekebisho.
Taasisi alizokutana nazo ni pamoja
na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira nchini (NEMC),
Taasisi ya Nguvu za Atomiki, Mamlaka ya Chakula na Dawa na Mkemia Mkuu
wa Serikali.
No comments :
Post a Comment