Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
21/04/2017
Kihistoria Tanzania ina mahusiano
mzuri na jirani zake, katika miaka ya hivi karibuni imekuwa ikishiriki
kwa ukamilifu katika juhudi za kuhimiza usuluhishi wa migogoro kwa njia
ya amani.
Sera ya Nchi za Nje ya Tanzania
inalenga kupanga, kukuza na kulinda maslahi ya kisiasa, kiuchumi,
kijamii na kiutamaduni kwa kutumia kikamilifu na kwa uendelevu
diplomasia ya
kiuchumi, kuhakikisha uhusiano wake na mataifa mengine,
taasisi za kimataifa unazingatia maslahi ya kiuchumi, kujenga uchumi wa
kujitosheleza, kudumisha amani na usalama wa taifa pamoja na kusaidia
jitihada za kikanda na kimataifa kwa ajiili ya kuhakikisha kunawapo
ulimwengu bora wenye amani.
Hakika palipo na nia pana njia,
nia njema ya kiongozi wa nchi ndio taswira halisi ya taifa katika kujali
utu, mwandishi wa makalama haya anaunga mkono utayari wa kiongozi wa
nchi kwa kujali watu ambao wapo tayari kuitangaza Tanzania nje ya mipaka
yake kwa kufanyakazi ya kuokoa maisha ya watu wa mataifa mengine
kulingana na sera yake.
Msukumo wa sera ya nchi
umewapelekea Watanzania kuthamini taaluma zao na kuwa tayari kuitendea
haki taaluama ya udaktari bila kujali mipaka ya nchi kwa ajili ya
kujenga mahusiano mema na nchi nyingine, huo ni moyo wa kizalendo kwa
taifa na watu wake.
Nichukue fursa hii kumpongeza
kwanza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe
Magufuli kwa utayari wake wa kujenga mahusiano mazuri na nchi jirani kwa
tayari kwa utayari wake wa kutoa Madaktari kwenda kufanyakazi nchini
Kenya.
Huo ni moyo wa kizalendo na utu
ambao unapaswa kuigwa na wakuu wa nchi nyingine kuwa tayari kusaidia
inapotokea uhitaji wa jambo fulani maana akufaaye wakati wadhiki ndiye
rafiki, ni vema majirani wasaidiane ili kutoa huduma hitajiwa kwa haraka
na kwa gharama nafuu kwa manufaa ya taifa.
Ni dhahiri jemedari Rais Dkt.
Magufuli akiwa pia Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ameonesha
nia ya dhati ya kuhudumia wananchi ndani ya jumuiya hiyo kwa kuwa tayari
kutoa madaktari 500 kulingana na maombi ya Serikali ya Kenya.
Hakika madaktari Watanzania
wapatao 496 waliwasilisha maombi yao, baada ya kufanyiwa uchambuzi
ilibainika Madaktari 258 na wataalamu wa Afya 11 ndio walikidhi vigezo
vinavyotakiwa kwenda kufanya kazi nchini Kenya.
Kwa mujibu wa Waziri wa afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati wa
mkutano wake na waandishi wa habari hivi karibuni mjini Dodoma,
amethibitisha kuwa Serikali imeamua kuwaajiri madaktari hao 258 waweze
kutoa huduma nchini badala ya kwenda kufanya kazi nchini.
Hatua hiyo ya Serikali ya Tanzania
ya kuwaajiri madaktari hao imefikiwa baada ya madaktari wa Kenya watano
kuwasilisha pingamizi mahakamani kuitaka Serikali ya nchi yao kusitisha
kuajiri Madaktari kutoka Tanzania.
“Kwa upande wetu sisi ratiba ya
utekelezaji wa ajira hizi za madaktari hao ilikubalika na pande zote iwe
tarehe 6 Aprili 2017 madaktari hao wawe tayari kusafiri kwenda nchini
Kenya kati ya tarehe 6 hadi 10 Aprili 2017. Hadi tarehe ya taarifa hii
Mahakama nchini Kenya haijaondoa pingamizi lililofunguliwa kuhusu ajira
za madaktari wa Tanzania nchini Kenya” alisisitiza Waziri Ummy.
Hakika uamuzi huo ni wa busara
unaosimamia kujali utu wa watu bila kujali mipaka, kwa dhamiri hiyo na
uamuzi Serikali, Madaktari hao watapangiwa vituo wawe tayari kwenda
kufanyakazi yao ya kusimamia afya za Watanzania ili waweze kuwa na afya
bora inayowawezesha kufanyakazi kwa juhudi na maarifa kwa maendeleo
endelevu.
Msingi wa madaktari wa Tanzania
kwenda kufanya Kenya ulitokana na nia ya Serikali Serikali ya Kenya
kupitia ujumbe wa uliofika nchini Machi 18, 2017 ukiongozwa na Waziri wa
Afya Dkt. Cleopa Mailu kuonana na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa
madhumuni ya kumuomba kuajiri kwa Mkataba Madaktari wa Tanzania ili
kupunguza uhaba wa Madaktari nchini Kenya na kukubali ombi hilo.
Utayari wa Rais Dkt. Magufuli
unakwenda sanjari na maneno ya aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Umoja Umoja
wa Mataifa Boutros Boutros-Ghali kupitia Mkataba wa umoja huo ambapo
aliwahi kusema “…….Umuhimu wa ushirikiano wa kimataifa ni kudumisha
amani na kuleta maendeleo, haki za binadamu, kuanzisha mazingira
yatakayowezesha kupatikana kwa demokrasia, kukuza maendeleo ya kijamii
na kuleta maisha bora”.
Kwa mujibu wa Shirika la Afya
Duniani (WHO) kupitia Mkutano wa Kimataifa wa Afrika juu ya Agenda Afya
(AHAIC) ulifanyika Machi 7, 2017 Nairobi, nchini Kenya, yaliwekwa
malengo kuwa Serikali za nchi za Afrika zinatakiwa kufanya utafiti
katika sekta ya afya kwa kuwashirikisha vijana na watendaji wengine na
kuweka nguvu ya pamoja katika kushughulikia matatizo ya magonjwa ndani
ya bara la Afrika ambapo Tanzania ilitumia fursa hiyo ili kudumisha
ushirikiano na jirani zake.
Aidha, ushirikiano unaooneshwa na
Serikali ya Tanzania kwa mataifa mengine umejikita katika usemi wa
Shirika la Afya Duniani unaohimiza mataifa yote kuwa “Kwa pamoja
tujitahidi kupambana na magonjwa” ili kujenga afya bora kwa ajili ya
watu wote duniani kwa kushirikiana na Serikali na Washirika wengine
katika kuhakikisha watu wote wanapata huduma bora za afya.
No comments :
Post a Comment