Na. Lilian Lundo – MAELEZO
Mabadiliko ya Tabianchi ni moja ya eneo ambalo limekuwa likileta athari kubwa katika nchi nyingi Duniani
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar zimeweka mikakati mbalimbali
katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.
Moja ya mikakati hiyo ni pamoja na
ujenzi wa kuta kwenye Pwani ya Bahari ya Hindi, upandaji wa mikoko
ikiwa ni pamoja na uchimbaji wa mifereji ya maji ya mvua na maji machafu
Akitoa taarifa kwa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira, Mkurugenzi Idara
Mazingira, Ofisi ya Makamu wa Rais, Richard Muyungi anasema Mradi wa
kujenga uwezo wa kuhimili athari za mabadiliko ya tabianchi katika Pwani
ya Bahari ya Hindi jijini Dar es Salaam unatekelezwa katika maeneo
manane na unagharimu dola za kimarekani milioni tano..
Bwana Muyungi anasema maeneo
ambayo mradi huo unatekelezwa kuwa ni eneo la Obama Ocean Road,
Kigamboni kwenye Chuo cha Kumbukumbu cha Mwalimu Nyerere, Bungoni Ilala,
Miburani Mtoni, Temeke, Salender Bridge, Kunduchi, Mbweni na Ununio
Kinondoni.
Anasema jumla ya Dola za Marekani
3,489,482 zimetengwa kwa ajili ya miundombinu ya ujenzi wa ukuta eneo
la Ocean Road na Kigamboni pamoja na mitaro iliyopo Bungoni, Ilala na
Mtoni Temeke
Katika ziara hiyo Bwana Muyungi
anazitaja shughuli nyingine zinazotekelezwa katika mradi huo ni pamoja
na kukarabati ukuta wa bahari katika maeneo ya barabara ya Obama ambayo
zamani ilijulikana kama Ocean Road wenye urefu wa mita 820 na
Kigamboni eneo la Chuo cha Kumbukumbu cha Mwalimu Nyerere, urefu wa mita
380, ambapo ukuta huo utadumu kwa zaidi ya miaka 73.
Pamoja na matengenezo hayo, fedha
nyingine zitatumika kutoa mafunzo kuhusu nishati safi ya kurudisha
mikoko ekari 40 ya mwambao wa Pwani ya Bahari ya Hindi katika maeneo ya
Jiji la Dar es Salaam.
Kwa upande wake, Mkurugenzi
Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira Zanzibar (ZEMA), Sheha Mjaja anaeleza
miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
(SMZ) kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni
pamoja na mradi wa kujenga uwezo wa kuhimili athari za mabadiliko ya
Tabianchi katika maeneo ya ukanda wa Pwani (mradi wa LDCF).
“Mradi huu unatekelezwa na
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Ofisi ya makamu wa
Rais katika maeneo ya Bagamoyo, Pangani, Rufiji na Zanzibar na
unafadhiliwa na Mfuko wa Dunia wa Mazingira (The Global Environmental
Facility- GEF) kupitia dirisha la Mfuko wa Nchi Masikini Duniani (The
Least Developed Countries Fund – LDCF) la Mkataba wa Mabadiliko ya
Tabianchi – UNFCCC,” anafafanua Sheha Mjaja.
Anafafanua kuwa fedha za Mradi
huo zinapitia Shirika la Usimamizi wa Mazingira la Umoja wa Mataifa
(UNEP) ambalo pia lina jukumu la kutoa ushauri wa kitaalamu na usimamizi
wa fedha na Jumla ya Dola za Kimarekani milioni 3,356,300 zimepangwa
kutumika katika mradi huu zikijumuisha fedha za usimamizi na ufuatiliaji
za UNEP ambapo Utekelezaji wa Mradi huu ulianza mwaka 2013 na
unategemewa kumalizika mwaka 2017.
Mkurugenzi mkuu huyo wa ZEMA
amezitaja shughuli zitakazofanyika katika mradi huo ni upandaji wa
mikoko/mikandaa na miti ya ukanda wa pwani katika maeneo 6 ya Unguja na
Pemba pamoja na ujenzi wa kuta za bahari katika eneo la Kilimani mjini
Unguja na Kisiwa Panza, wilaya ya Mkoani Pemba.
Anafafanua kuwa, eneo la Kilimani
ambalo ufukwe wake una urefu wa mita 538 litajengwa kuta mbili (2) za
aina ya “gyrones”,ambapo kila ukuta utakuwa na urefu wa mita 100 kutoka
kwenye fukwe kuelekea
No comments :
Post a Comment