Na Mahmoud Ahmad Kondoa
Sintofahamu imeibuka upya katika
mgogoro wa Kikundi cha wachimbaji wadogo wa madini na kampuni ya Kidee
Minning (T) Ltd katika eneo la Kata ya Changaa baada ya viongozi na
watendaji wa serikali kudai hawana taarifa za uwepo wa kikundi hicho.
Kadhia hiyo imeibuka baada ya
kuwepo malalamiko ya kuvamiwa kwa kikundi kinachoendesha shughuli za
utafiti na uchimbaji wa madini,utunzaji wa mazingira,ufugaji wa
nyuki na
ujasiriamali na kutambuliwa na mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya
Kondoa.
Aidha ofisi ya Kitongoji cha
changaa iliyobariki kupitia ofisi ya kata kupata hati ya utambuzi wa
kikundi imeonekana viongozi wa kata na kitongoji kukanusha vikali mbele
ya halmashauri ya wilaya ya kondoa kuwa hawakitambui kikundi cha Kumucha
wakati mkurugenzi anakitambua na kutoa hati ya kikundi hicho june mwaka
2015.
Hata hivyo uongozi huo wa kata na
kitongoji wametoa muhtasari halali kupitia mkutano mkuu wa kijiji kwa
wakati huo na kikundi kubarikiwa kuendelea na kupata ridhaa ili kupata
hati ya utambuzi wa kikundi hicho kupitia ofisi ya mkurugenzi wa
halmashari ya Kondoa.
Akizungumza na mwanahabari hii
diwani Issa Bou na Mwenyekiti wa kitongoji Kenyeta Fonda wamenukuliwa
wakikitambua kikundi hicho lakini kwenye mamlaka husika wakikikataa
ambapo diwani huyo ni mlezi wa kikundi hicho.
Dodoso za wanahabari hii zimeenda
mbali baada ya kubaini kuwepo kwa ukiukwaji na matumizi mabaya ya ofisi
za serikali kupitia viongozi hao kwa kutumia serikali ya kijiji
kupitisha masuala mbali mbali yenye manufaa bila kuwashirikisha wananchi
na kutoa maamuzi binafsi.
Mfano wa suala la utunzaji wa
mazingira, serikali ya kijiji imewahukumu mmoja ya wanakikundi
aliyenunua miche ya miti na kwenda kuipanda kwenye eneo lililoharibiwa
kwa ukatwaji wa miti na kuchoma mkaa na kumuhuku kifungo cha miaka
miwili jela au kulipa faini ya tsh.200,000
Aidha ndipo alipoamua kuilipa
serikali ya kijiji hicho faini hiyo bila kupewa stakabadhi ya ofisi
ambapo alifuatilia kupewa risiti hadi leo bila mafanikio na ndipo
ilipojitokeza hali ya kutaka kumridhisha kwa kumruhusu kuendelea na
kusudio lake la upandaji wa miti ambapo awali walingoa miche aliopanda
kwa madai ya kuwa eneo hilo si mali yake ni mali ya kijiji.
Nae Mwenyekiti wa Kumucha
Donmillan Shirima amesema kuwa kumekuwapo na sintofahamu hiyo ambapo
juzi mwekezaji amefyeka miti na kuharibu mazingira bila taarifa ambapo
serikali ya mtaa wa tumbelo na kitongoji Changaa wakitupiana mpira
katika suala hilo juu ya nani mhusika wa eneo hilo.
Amesema kuwa suala hilo lipo
kwenye mamlaka husika ambapo serikali ya wilaya inalifanyiakazi na wao
kwa sasa hawana la kuzungumza wanasubiria majibu ya msingi ya malalamiko
yao ya uvamizi wa eneo lao,
Shirima amesema kuwa mamlaka
husika na vijiji zimekuwa zikiwataka kukaa mezani na mwekezaji wakati
wao wanahitaji tafsiri ya utambuzi wao na uhalali wa uwepo wa kisheria
katika eneo hilo.
No comments :
Post a Comment