Serikali kupitia Wizara ya
Elimu,Sayansi na Teknolojia imelipa madeni ya fedha za likizo kwa walimu
86,234 kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2015/2016 na 2016/17.
Hayo yamebainishwa na Naibu
Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Mhe.Stella Manyanya wakati akijibu
hoja mbalimbali za wabunge Mjini Dodoma.
“Serikali inaendelea kulipa
madeni mbalimbali ikiwa ni pamoja na fedha za likizo kwa
walimu/Watumishi katika sekta ya Elimu”,Aliongeza Mhe.Manyanya.
Amesema kuwa katika kipidi cha
mwaka wa fedha 2015/16 hadi mwezi Juni, 2016 jumla ya
shilingi bilioni
22,629,352,309 zililipwa kwa walimu 63814, na pia katika kipindi cha
mwaka wa fedha 2016/17 hadi kufikia mwezi Machi, 2017 jumla ya shilingi
bilioni 10,505,160,275 zimelipwa kwa walimu 22420.
Aidha katika malipo haya jumla ya
shilingi 13,415,410 zimelipwa kwa ajili ya madeni ya fedha za likizo
kwa watumishi wa chuo cha ualimu Korogwe.
Akizungumzia upande wa
upandishaji madaraja Mhe.Manyanya amesema kuwakwa sasa uhakiki wa
watumishi unaendela na ukikamilika watapandisha madaraja kama
inavyotakiwa.
Aidha amesisitiza kuwa Wizara ya
Elimu,Sayansi na Teknolojia imekuwa ikiwapandisha vyeo watumishi wake
wenye sifa kila mwaka ambapo katika mwaka 2015/16 Wizara iliwapandisha
vyeo watumishi 2272 kati yao watumishi 71 ni wa chuo cha ualimu korogwe.
Uhakiki wa madeni ya miaka ya
nyuma unaendelea kuratibiwa na mamlaka husika na taratibu za malipo
zitakamilishwa kwa wale wanaostahili.
No comments :
Post a Comment