Wizara ya Maji na Umwagiliaji
imesema kuwa mkandarasi ameanza kazi ya ujenzi wa mabomba ya usambazaji
katika maeneo ya Malamba Mawili,Msigani,Mbezi
Luisi,Msakuzi,Kibamba,,Kiluvya,Mloganzila na Mailimoja na atakamilisha
kazi hiyo mwaka huu 2017.
Hayo yamesemwa leo Bungeni Mjini
Dodoma na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji
Mhe.Isack Kamwelwe wakati
akijibu hoja mbalimbalia za wabunge.
“Baada ya kukamilika kwa mradi
maeneo mengi ndani ya kilomita 12 ya pembezoni mwa bomba kuu la Ruvu
Juu yameanza kupata huduma ya Maji”,Aliongeza Mhe.Kamwelwe.
Amesema kuwa maeneo ambayo
yanapata maji kwa sasa kutoka Bomba la Ruvu Juu ni pamoja na Mlandizi na
vitongoji vyake, Visiga, Misugusugu, Soga, Korogwe, Picha ya Ndege, Kwa
Matiasi,Tumbi, Mailimoja, Pangani, Kiluvya, Kibamba, Mloganzila, Mbezi
kwa Yusufu,Mbezi Mwisho, Kimara, Mavurunza, Baruti, Kibo,
Kibangu,Tabata, Segerea, Kinyerezi na Karakata.
Aidha maeneo ambayo bado
hayajaanza kupata huduma ya maji yatapata huduma hiyo baada ya
utekelezaji wa miradi mipya ya kujenga mtambo wa mabomba ya kusambaza
maji katika maeneo yote ambayo hayana huduma hiyo, Amesema kuwa miradi
hii itatekelezwa kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha .
No comments :
Post a Comment