Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
KUNDI la watu
wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wamevamia kiwanda cha prayose wilayani
Kisarawe mkoani Pwani na kupora fedha na mali zenye thamani ya mil. 25.
Kati ya vitu
vilivyoporwa ni pamoja na fedha taslimu sh mil. 18,laptop mbili za mil.
mbili na simu 14 zenye gharama ya mil. tano.
Aidha katika tukio
hilo watu wanne wenye asili ya kihindi wamejeruhiwa kwa kupigwa na nondo
kwenye maeneo mbalimbali ya miili yao.
Kufuatia tukio hilo jeshi la polisi mkoani Pwani, linawashikilia walinzi waliokuwa zamu kwa mahojiano.
Kamanda wa polisi
mkoani hapo, kamishna msaidizi mwandamizi, Onesmo Lyanga, alithibitisha
kutokea kwa tukio hilo, april 13 majira ya saa 7 usiku .
Alisema huko maeneo
ya kiwanda hicho, kundi la watu zaidi ya sita wakiwa na mapanga na
marungu walikivamia na kuwafunga kamba walinzi wawili waliokuwa zamu
kisha kuingia ndani ya kiwanda na kujeruhi wahindi wanne.
Kamanda Lyanga
alieleza, licha ya kuwajeruhi watu hao ,waliweza kuwafunga kwa kamba
wafanyakazi waliokuwa wakiendelea na uzalishaji kiwandani ambapo
walifanikiwa kupora mali na fedha.
Alitoa rai kwa
wafanyabiashara kuacha kuhifadhi kiwango kikubwa cha fedha ndani na
badala yake fedha hizo wakazihifadhi kwenye taasisi za kifedha -bank kwa
usalama zaidi.
“Wafanyabiashara wajitambue kwani kuweka fedha ndani, kwenye kampuni ni risk “
“Kufuatia suala hilo lilivyo tunawashikilia walinzi wa kampuni hiyo kwa uchunguzi zaidi “alisema.
Kamanda Lyanga aliomba ushirikiano kwa jamii kulisaidia jeshi hilo mara watakapobaini watu waliofanya tukio hilo
No comments :
Post a Comment