Mwenyekiti wa Bodi ya Zabuni ya
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Kamishna wa Fedha na
Utawala wa Magereza, Gaston Sanga (watatu kushoto), Katibu wa Bodi hiyo
ambaye pia ni Mkurugenzi wa Manunuzi wa Wizara hiyo, David Mwangosi
wakimsikiliza Mkuu wa Kitengo cha Majengo wa Idara ya Uhamiaji, Hamza
Shabani (kushoto), wakati wajumbe wa Bodi hiyo walipotembelea nyumba za
makazi za Makamishna wa Uhamiaji, Mtoni Kijichi, jijini Dar es Salaam.
Bodi hiyo ilitoa wiki tano kwa Kampuni ya Ujenzi ya Koberg kukamilisha
ujenzi wa nyumba hizo.
Katibu wa Bodi ya Zabuni, Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia Mkurugenzi wa Manunuzi wa Wizara
hiyo, David Mwangosi akiwafafanulia jambo Wajumbe wa Bodi ya Zabuni ya
Wizara hiyo, wakati wajumbe hao walipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa
nyumba za makazi ya makamishna wa Uhamiaji zilizopo Mtoni Kijichi,
jijini Dar es Salaam. Hata hivyo, Wajumbe wa Bodi hiyo walitoa wiki tano
kwa Kampuni ya Ujenzi ya Koberg kukamilisha ujenzi wa nyumba hizo.
Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo, ambaye pia ni Kamishna wa Fedha na
Utawala wa Magereza, Gaston Sanga.
Mwenyekiti wa Bodi ya Zabuni,
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Kamishna wa Fedha na
Utawala wa Magereza, Gaston Sanga (kushoto) akiangalia kabati la nguo
katika moja ya chumba cha nyumba za makamishna wa Uhamiaji zilizopo
Mtoni Kijichi, jijini Dar es Salaam. Wajumbe wa Bodi hiyo walizikagua
nyumba hizo na kutoa wiki tano kwa Kampuni ya Ujenzi ya Koberg
kukamilisha ujenzi.
Mkuu wa Kitengo cha Majengo wa
Idara ya Uhamiaji, Hamza Shabani akiwaonyesha Wajumbe wa Bodi ya Zabuni
ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, nyumba za makazi za makamishna wa
Uhamiaji zilizopo Mtoni Kijichi, jijini Dar es Salaam. Wapili kushoto ni
Mwenyekiti wa Bodi hiyo, ambaye pia ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa
Magereza, Gaston Sanga. Wapili kulia ni Katibu wa Bodi hiyo ambaye pia
ni Mkurugenzi wa Manunuzi wa Wizara hiyo, David Mwangosi, watatu kulia
ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Uhamiaji, Peter Chogero, na kulia ni
Mhasibu Mkuu wa Wizara hiyo, Edwin Makene.
Mhandisi wa Kampuni ya Ujenzi ya
Koberg ambayo inajenga nyumba za makazi za Makamishna wa Idara ya
Uhamiaji, Leonard Leonidace, akiwafafanulia jambo Wajumbe wa Bodi ya
Zabuni ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, walipozitembelea nyumba hizo
wakikagua maendeleo ya ujenzi wa nyumba hizo, hata hivyo Wajumbe wa
Bodi walitoa wiki kwa Kampuni hiyo kukamilisha ujenzi. Kulia ni
Mwenyekiti wa Bodi ya Zabuni, Wizara hiyo ambaye pia ni Kamishna wa
Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga, na wanne kulia ni Katibu wa
Bodi hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Manunuzi wa Wizara hiyo, David
Mwangosi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Zabuni,
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Kamishna wa Fedha na
Utawala wa Magereza, Gaston Sanga (Katikati) na Katibu wa Bodi hiyo
ambaye pia ni Mkurugenzi wa Manunuzi wa Wizara hiyo, David Mwangosi
(wanne kulia), wakiwa
katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi hiyo,
mara baada ya wajumbe hao kumaliza ziara yao ya kukagua ujenzi wa nyumba
za makazi za Makamishna wa Idara ya Uhamiaji, zilizopo Mtoni Kijichi,
jijini Dar es Salaam. Hata hivyo, Wajumbe wa Bodi hiyo walitoa wiki tano
kwa Kampuni hiyo kukamilisha ujenzi wa nyumba hizo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Bodi ya Zabuni ya Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi, imeipa muda wa wiki tano Kampuni ya Ujenzi ya Koberg
Construction Co.Ltd kukamilisha ujenzi wa nyumba za makazi za
Makamishna wa Idara ya Uhamiaji hapa nchini zilizoko katika eneo la
Mtoni Kijichi jijini Dar es Salaam ambazo zitatumiwa na Makamishna hao.
Uamuzi wa Bodi hiyo umekuja baada
ya Kampuni ya Koberg Construction ya nchini hapa kuonyesha kusuasua na
kushindwa kukamilisha ujenzi wa nyumba hizo kwa wakati.
Bodi hiyo inayoongozwa na
Mwenyekiti wake Kamishna wa Utawala na Fedha wa Jeshi la Magereza,
Gaston Sanga na Katibu wake Bw. David Mwangosi ambaye pia ni Mkurugenzi
wa Kitengo cha Manunuzi cha Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, imefanya
maamuzi hayo baada ya kufanya ukaguzi na kujionea hatua zilizofikiwa
katika ujenzi wa nyumba hizo.
Kwa upande wake Katibu wa Bodi
hiyo amesema kitendo cha Mkandarasi huyo kusuasua kukamilisha kwa wakati
kazi ya ujenzi wa nyumba hizo ulioanza tangu mwaka wa Fedha wa
2014/2015 ndicho kilichoifanya Bodi ya Zabuni ya Wizara hiyo kuamua
kutembelea eneo ambalo kazi ya ujenzi wa nyumba hizo unaendelea na
kumpatia wiki tano tu kuhakikisha anakamilisha kazi hiyo.
********************
No comments :
Post a Comment