Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa
akizungumza viongozi wa kiwanda cha nguo cha Mauritius cha Compagnie
Mauricienne De Textile Ltee baada ya kutembelea kiwanda hicho kilichopo
nje kidogo ya mji wa Port Louis Machi 22, 2017. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akitazama nguo zilizoshonwa kwa vitambaa vilivyotengenezwa na kwanda
cha nguo cha Compagne Mauricienne De Textile Ltee cha Mauritius wakati
alipotembelea kiwanda hicho, nje kidogo ya mji wa Port Louis nchini
Mauritius, Machi 22, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kasim Majaliwa
akitazama mitambo ya kiwanda cha kuengeneza nyuzi za pamba wakati
alipotembelea kiwanda cha nguo cha Compagne Mauricienne De Textile Ltee
kilichopo nje kidogo ya mji wa Port Louis nchini Mauritious. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)

……………………………………………………………………………………………..
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
ametembelea kiwanda cha Compagnie Mauricienne De Textile Ltee
kinachotengeneza nguo kwa kutumia teknolojia ya kisasa nchini Mauritius
chenye uwezo wa kutengeneza tani milioni 40 hadi 50 kwa mwaka.
Aidha, Waziri Mkuu alitumia fursa
hiyo kuwakaribisha wawekezaji hao kuja nchini Tanzania na kuwekeza
katika viwanda vya kutengeneza nyuzi pamoja na nguo kwa kuwa kuna
malighafi
za kutosha kwa ajili ya uzalishaji huo.
Waziri Mkuu alitembelea kiwanda
hicho kilichoko katika mji wa Latour Koenig jana (Jumatano, Machi 22,
2017) na kujionea namna wanavyotengeneza nguo kwa kutumia teknolojia ya
kisasa na kuamua kuwakaribisha waje kuwekeza nchini.
“Tumefarijika na uwekezaji wenu
na tumejionea namna ambavyo mnavyoendesha kiwanda chenu kuanzia
utengenezaji wa nyuzi hadi nguo, hivyo tunahitaji viwanda kama hivi
nchini Tanzania kwa sababu sisi tunazalisha pamba nvingi na yenye ubora
unaokubalika kimataifa,” alisema.
Waziri Mkuu alisema madhumuni ya
kuwakaribisha wawekezaji hao kuja Tanzania na kuwekeza katika viwanda
vya kutengeneza nyuzi yanalenga kuboresha kilimo cha pamba na
kuwawezesha wakulima kupata tija.
“Tunalima pamba nzuri na hawa
hawalimi wananunua kutoka nje ya nchi yao, hivyo wakija kuwekeza
Tanzania itawarahisishia kupata malighafi ya uhakika na kwa urahisi ”
alisema.
Alisema viwanda hivyo vitasaidia
maendeleo ya kilimo cha pamba kwa sababu vitatoa ajira kwa wananchi
wengi hivyo kuwawezesha kujikwamua kiuchumi na kuondokana na umasikini
wa kipato.
Mbali na kuwakaribisha wawekezaji
hao, pia Waziri Mkuu alitoa wito kwa wananchi wenye uwezo kuhakikisha
wanajenga viwanda vya nyuzi kwenye mikoa yote inayozalisha pamba ili
waweze kuiongezea thamani kabla ya kuiuza.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa
Fedha wa kiwanda hicho Bw. David Too Sai Voon alisema wamefurahishwa na
mualiko wa kuja Tanzania kwa ajili ya kuangalia maeneo ya uwekezaji wa
viwanda vya nyuzi na nguo.
Bw. David alisema kiwanda chao
kilianzishwa mwaka 1986 na kwa sasa kimeajiri wafanyakazi 18,000 ambapo
mauzo yao kwa ni dola milioni 200. “Nguo tunazotengeza ni za kiwango cha
kimataifa na tunauza katika maduka makubwa barani Ulaya,”
No comments :
Post a Comment