Afisa
mtendaji mkuu na mwanzilishi wa kampuni ya NINAYO Jack Langworthy
akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari juu ya kuanzisha
ushirikiano baina ya kampuni hiyo na shirika lisilo na kiserikali la
Heifer utakaowawezesha wakulima kufikia masoko kupitia njia ya mtandao
wa www.NINAYO.com .Kushoto ni Mkurugenzi mkazi wa Heifer International Tanzania Bi. Leticia Mpuya.
Meneja
uendeshaji wa kampuni ya NINAYO Bovan Mwakyambiki akiungumza katika
mkutano na waandishi wa habari juu ya kuanzisha ushirikiano baina ya
kampuni hiyo na shirika lisolo na kiserikali la Heifer International
Tanzania utakaowawezesha wakulima kufikia masoko kupitia njia ya mtandao
www.NINAYO.com Kulia ni Afisa mtendaji mkuu na mwanzilishi wa kampuni ya NINAYO Jack Langworthy.
Mkurugenzi
mkazi wa Heifer nchini Bi. Leticia Mpuya akiungumza katika mkutano na
waandishi wa habari juu ya kuanzisha ushirikiano baina ya shirika hilo
na kampuni ya NINAYO utakaowawezesha wakulima kufikia masoko kupitia
njia ya mtandao wa www.NINAYO.com Kulia ni Afisa mtendaji mkuu na mwanzilishi wa kampuni ya NINAYO Jack Langworthy.
Tarehe 22 Machi 2017, Dar es
salaam. Kampuni ya Ninayo kwa kushirikiana na shirika lisilo la
kiserikali la Heifer International Tanzania ambalo limejikita katika
kuondoa umasikini na matatizo ya njaa leo wameshirikiana katika
kuwasaidia wakulima wa Tanzania kupata taarifa zote zinazohusu mauzo au
manunuzi ya mazao mbalimbali kupitia mtandao wa Ninayo.com.
Ninayo ni jukwaa la mtandao wa
kibiashara unaowawezesha wakulima kuuza, kununua au kuangalia bei
elekezi za mazao mbalimbali yatokanayo na kilimo pia kuwapa uwanja mpana
wa kulifikia soko la bidhaa hizo kwa urahisi.
Njia hii ya mtandao imejikita
katika kutatua mambo makubwa matatu ikiwemo tatizo la kushindwa kwa
mkulima katika usambazaji ambapo wanunuaji/wateja hawafahamu ni mazao ya
aina gani wakulima wanauza, Mahitaji yasiyofahamika ambapo wakulima
hawafahamu ni kiasi gani wanunuaji wapo tayari kununua mazao yao na
kukosekana kwa utaratibu wa kuwaunganisha wanapohitaji kufanya biashara
za mazao yao.
Akizungumza kwenye mkutano na
waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam, Mwanzilishi na Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Ninayo Jack Langworthy alisema matumizi ya
intaneti yanazidi kukua kwa kasi sana nchini Tananzia, na hivi sasa
intaneti imesambaa hadi vijiji maskini.
“Tunashukuru kwa kukua kwa kasi
ya mitandao hasa kupitia simu za mkononi, ni uvumbuzi ambao umeleta
mapinduzi katika kila sekta duniani, kuanzia kwenye bishara ya teksi,
hoteli na zaidi sasa inaweza kupatikana kwa wakulima katika masoko ya
Tanzania kukabiliana na mahitaji mahitaji mbalimbali ya chakula kwa bei
elekezi kwa watu wote na hivyo kupunguza upotevu wa mazao mbalimbali”.
Ninayo itasaidia kuwaunganisha
wakulima kwa pamoja katika soko rasmi, na itaweka bei elekezi kwenye
biashara ya mahindi, maharage, ndizi, maembe, matikiti maji pamoja na
bidhaa nyingine nyingi za kilimo katika kuleta uwazi na ukweli wa bei ya
soko na hivyo kuwawezesha wakulima kujivunia mazao yao.
Aliongeza kuwa Ninayo mpaka sasa
imefanikiwa kuwaunganisha wakulima wa mikoa kama Iringa, Mbeya, Morogoro
na Njombe pamoja na wanunuaji wa bidhaa zao, jambo lilisaidia kuongeza
kipato chao.
Aliendelea kusema kuwa Ninayo
inaunganisha hadi wakulima wasio na uwezo wa kupata intaneti kwa kupitia
njia ya ujumbe mfupi wa maneno.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa
Heifer International Tanzania Bi. Leticia Mpuya alipongeza juhudi
zinazofanywa kupitia mtandao huo akisema itasaidia kuwaunganisha
wakulima na wateja wao nchini na Afrika mashariki yote.
Ushirikiano kati ya Ninayo na
Heifer International ni katika kuelimisha wakulima jinsi ambavyo
wanaweza kunufaika kwa kuuza mazao yao kwa kupitia mtandao huo. Heifer
ambao wanafanya kazi na mamia ya wakulima nchini itawasaidia wakulima
wake kutumia mtandao wa Ninayo ili waweze kujipatia faida kwa
kuhakikisha wanauza bidhaa zao kwa bei za kujiridhisha.
“Kama shirika linalohusika na
kutokomeza njaa na umaskini, huwa tunakabiliwa na changamoto mbalimbali
katika kuhakikisha wakulima wanauza mazao yao kulingana na bei zilizo za
kibiashara na kwa manufaa kwao pia kupata wanunuzi sahihi na hivyo
kupitia mtandao huu utasaidia kusulisha changamoto hiii” alisema.
No comments :
Post a Comment