Frank Mvungi-Maelezo
Watumishi wa Umma wametakiwa
kuzingatia maadili na kuacha kutumia madaraka yao vibaya kwa maslahi
binafsi hali inayoweza kuzorotesha huduma wanazotoa kwa wananchi.
Onyo hilo limetolewa na Mkuu wa
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Kinondoni
Bw. Benn Lincoln kufuatia kukamatwa kwa Afisa Afya wa Kata ya Mbweni
Manispaa ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam Bw. Amos Ndalawa kwa makosa
ya kuomba na kupokea rushwa.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa
na TAKUKURU, mshtakiwa huyo alifikishwa kwenye Mahakama ya Wilaya ya
Kinondoni na kufunguliwa mashtaka mawili ya kuomba na kupokea rushwa
kinyume na kifungu namba 15(1)(a) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa namba 11 ya mwaka 2007.
Mwendesha mashitaka wa TAKUKURU
Bibi. Vera Ndeoya aliieleza Mahakama kuwa mshitakiwa akiwa mwajiriwa wa
Halmashauri ya Kinondoni kama Afisa Afya wa Kata ya Mbweni mnamo tarehe
21 Machi, 2017 alishawishi na kupokea rushwa ya shilingi laki 3 kutoka
kwa Leticia Lubala ili asimchukulie hatua za kisheria baada ya kukagua
biashara yake. Ilisisitiza sehemu ya taarifa hiyo.
Taarifa hiyo iliongeza kuwa kesi hiyo imeahirishwa hadi Aprili 10 mwaka huu kwa vile uchunguzi haujakamilika.
No comments :
Post a Comment