Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe akisalimiana na Msanii wa Muziki
wa kizazi kipya Emmanuel Elibariki maarufu kama Ney wa Mitego kwa
mwaliko Ofisini kwake Mjini Dodoma kufanya mazungumzo yahusuyo mambo ya
Sanaa ya Muziki.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya
Emmanuel Elibariki maarufu kama Ney wa Mitego akitia saini katika kitabu
cha wageni mara baada ya kuwasili katika Ofisi ya Waziri wa Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe Mjini Dodoma kwa
mazungumzo.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe akisisitiza jambo kwa Msanii wa
Muziki wa kizazi kipya Emmanuel Elibariki maarufu kama Ney wa Mitego
mara baada ya mazungumzo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe akizungumza na waandishi wa
habari(hawapo pichani) mara baada ya kumaliza mazungumzo na Msanii wa
Muziki wa kizazi kipya Emmanuel Elibariki maarufu kama Ney wa Mitego
Ofisini kwake Mjini Dodoma.
Msanii wa Muziki wa kizazi kipya
Emmanuel Elibariki maarufu kama Ney wa Mitego akizungumza na waandishi
wa habari(hawapo pichani) mara baada ya kumaliza mazungumzo na Waziri wa
Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe Mjini
Dodoma.
Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM Dodoma.
………………..
Na Raymond Mushumbusi WHUSM Dodoma
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe ametoa wito kwa wasanii nchini
kutovuka mipaka katika utengenezaji wa kazi zao mpaka kufikia hatua ya
kuvunja Sheria na taratibu za nchi.
Ameyasema hayo Mjini Dodoma jana
alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukutana na
kufanya mazungumzo na Msanii wa muziki wa kizazi kipya Emmanuel
Elibariki maarufu kama Ney wa Mitego kwa mwaliko wa Waziri huyo.
Amesema kuwa wasanii ni nguzo
muhimu katika nchi sio kwa kufanya kazi ya kuburudisha na kuelimisha
bali katika kuujenga Utamaduni wa nchi ambao ndio nguzo muhimu sana kwa
malezi na makuzi ya wanajamii.
“Niwaombe wasanii nchini
kuzingatia Sheria na taratibu za nchi katika utunzi wao na utenegenezaji
wao wa kazi zao” Alisisitiza Mhe. Dkt Mwakyembe.
Aidha ameongeza kuwa Serikali
haina nia ya kuwanyima uhuru wa kujieleza bali watambue kuwa nchi
inaendeshwa kwa taratibu na Sheria ambazo zinatakiwa zifuatwe na watu
wote.
Kwa upande wake Msanii wa muziki
wa kizazi kipya Emmanuel Elibariki maarufu kama Ney wa Mitego
amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe
Magufuli kwa kuwaunga mkono wasanii nchini na kuahidi kuongeza baadhi
ya mambo katika wimbo wake wa “Wapo” na kuwaalika watanzania kama kuna
kero zingine zinazowasumbua katika jamii wasiwasilishe kwake ili
azizungumzie katika wimbo huo.
“Namshukuru Mhe. Rais kwa kutuunga
mkono pia naahidi kufanya “remix” ya wimbo wa “Wapo” kwa kuongeza
maneno niliyoshauriwa na Mhe Rais na Mhe. Waziri na kama kuna mengine
kutoka kwa wananchi pia niko tayari kuyapokea na kuyafanyia kazi”
alisema Bw. Elibariki.
Hivi karibuni wimbo wa “Wapo” wa
Msanii Emmanuel Elibariki maarufu kama Ney wa Mitego ulifungiwa Baraza
la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa kosa la kutozingatia maadili na baadae
kufunguliwa kwa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
John Pombe Magufuli kupitia Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo
Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe.
No comments :
Post a Comment