Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege
la ATCL, Bw. Lasislaus Matindi anasema wamefanikiwa kukusanya Shilingi
Bilioni 9 kwa Miezi minne tu kwa kutumia ndege hizo mbili zilizonunuliwa
na Rais Dkt. John Pombe Magufuli, nakuleta utata mkubwa na wapinzani wa
siasa nchini waliodai kuwa hazikuwa na tija kwa Taifa.
Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL)
ilianzishwa mwezi Novemba 2002 baada ya Serikali kubinafsisha lililokuwa
Shirika la Ndege la Tanzania (Air Tanzania Corporation, ATC); katika
Shirika hilo, Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA) lilinunua hisa
asilimia 49 ndani ya ATC. Hata hivyo ubia kati ya ATCL na SAA
ulikabiliwa na matatizo ya kiuendeshaji na kulazimika kusitishwa mwezi
Agosti 2006 na ATCL kurejeshwa tena Serikalini kwa asilimia 100.
KUMBUKUMBU:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt John Pombe Magufuli akiwa na maafisa na viongozi wengine mbalimbali
akikata utepe kuzindua rasmi ndege mbili mpya aina ya Bombadier Q400
zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Tanzania
(ATCL) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es salaam Jumatano
Septemba 28, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli pamoja na maafisa
wengine waandamizi wakiwa kwenye ndege mojawapo baada kuzindua rasmi
ndege mbili mpya aina ya Bombadier Q400 zilizonunuliwa na serikali kwa
ajili ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) katika Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Dar es salaam Jumatano Septemba 28, 2016.
PICHA NA IKULU.
No comments :
Post a Comment