Na Masanja Mabula –Pemba ..
WANANCHI wa wilaya ya Mkoani , Mkoa wa Kusini Pemba,
wameitaka Tume ya Kurekebisha Sheria Zanzibar, kuingiza kipengele cha
watoto wanaoanzia miaka 14 kulipwa fidia, wakati wanapopata ajali
wakiliokoa zao la karafuu.
Walisema
wachumaji wakubwa wa zao la karafuu ni watoto wenye umri kati ya miaka
14 hadi 17, hivyo ni vyema kwenye marekebisho ya sheria ya fidia, watoto
wenye umri huo wakatambuliwa na sheria ili kulipwa fidia wanapopata
ajali .
Hayo walieleza mbele
ya Tume ya Kurekebisha Sheria, inayoongozwa na Mwenyekiti wake Jaji
Mshibe Ali Bakari, wakati ilipokutana na wananchi hao, ili kukusanya
maoni yao, juu ya kuzifanyia mapitio sheria za usalama kazini na ile ya
fidia zote za mwaka 2005.
Maoni
ya wananchi hao, yalikuja kufutia sheria ya sasa ya fidia ya mwaka 2005
kwamba, haimtambui kifidia kwa mtu aliyeanguka wakati akichuma karafuu,
kama hajafikia umri wa miaka 18.
Mjumbe
wa mkutano huo Juma Bakar Shoka, alisema wachumaji hasa wa zao la
karafuu ni watoto wenye umri kuanzia miaka 14 na kuendelea, hivyo lazima
sheria iwatambue kulipwa fidia.
“Mimi
napendekeza kwenye sheria mpya ijayo ya fidia, na hawa watoto walipwe
fidia, maana ndio hasa wenyewe wanaozichuma karafuu na hata skuli wakati
mwengine hufungwa’’,alipendekeza.
Nae
Salum Omar alisema watu wenye umri mkubwa, wengi wao sio wachumaji hasa
wa zao taifa la karafuu, na badala yake watoto wenye umri wa kati, ndio
wahusika wakuu.
“Hata
mimi napendekeza sheria ya fidia ijayo, iwatambue watoto wenye umri
kuanzia umri wa miaka 14 na kuendelea, maana tukifanya kinyume chake,
tutawakosesha haki yao ya kujifunza kuchuma karafuu’’,alisema.
Kwa
upande wake Rashid Abdalla, alisema hata sheria inayokuja ielekeze wapi
fedha hizo zinapatikana na kusiwe na urasimu, na kumfanya mpatwa na
ajali kujuta kuzifuatilia.
Akifungua
mkutano huo Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Zanzibar Jaji
Mshibe Ali Bakar, alisema ingawa sheria za kimataifa zinakataza mtoto
kufanyishwa kazi zenye kuhatarisha maisha yake, lakini hilo
wataliangalia kwa ukaribu.
Katika
hatua nyengine Mwenyekiti huyo, alisema lengo la kuzifanyia marekebisho
sheria za fidia na ile ya usalama kazini za mwaka 2005, kuhakikisha
wananchi wote wanaishi kwa usawa.
Sheria
ambazo Tume ya Kurekebisha Sheria Zanzibar inazifanyia mapitio ni ile
sheria ya fidia ya kazini No 15 ya mwaka 1986 pamoja na marekebisho yake
ya mwaka 2005 na sheria ya usalama kazini No 8 ya mwaka 2005.
No comments :
Post a Comment