Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
VIONGOZI na wanachama wa
Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tisa kata ya Mjawa wilaya ya Kibiti,
wanadaiwa kuawa kwa kupigwa risasi na wengine kuchomwa moto kutokana na
matukio ya mauaji ya mfululizo yanayoendelea wilayani hapo .
Aidha CCM mkoa na Taifa
imeombwa kutupia macho suala hilo kwa upana na kulisimamia ili
kubaini
chanzo halisi kinachosababisha wauawe.
Kutokana na hali hiyo
wanachama wa maeneo ya wilaya hiyo, wanashindwa kuvaa sare za chama na
kuogopa kuitana majina ya vyeo vyao.
Mwenyekiti wa CCM kata
ya Mjawa ,Abubakar Seif, alisema baadhi ya viongozi wa vijiji na
vitongoji wanashindwa kwenda ofisini kutekeleza majukumu yao.
Akizungumza katika
mkutano wa ndani katika kata hiyo,ulioitishwa na chama hicho mkoa
alisema wanaishi kwa sintofahamu na imani inawatoweka.
Abubakar alisema watu wanakiogopa chama kwasasa na kukimbia miji na ofisi zao.
Anaeleza miaka ya nyuma watu walikuwa wakigombea nafasi mbalimbali za uongozi lakini kwa sasa wanakwepa na kuhofia uhai wao.
Abubakar alikiomba chama kiendelee kwa nguvu zake kutoa hamasa kwa wanachama wa Rufiji na Kibiti kurejesha amani kwa vijana.
“Ni mashaka makubwa kwanini wauwe viongozi wa CCM pekee, sawa kila mtu na umauti wake lakini si kihivii “
“Tatizo hapa ni masuala ya kisiasa ambapo ukanda huu unatawaliwa na mvutano wa kisiasa toka huko nyuma “alisisitiza.
Katibu wa CCM Kibiti, Zena Mgaya, alisema ulinzi ni wa kila mmoja ili kusaidiana na jeshi la polisi.
Aliomba waendelee kukipenda chama na kukisimamia kwani vitendo hivyo vinadhibitiwa kwasasa.
Zena alieleza
haiwezekani chama kikakaa bila viongozi wa chini, amewapa moyo wasikate
tamaa hali itakayosababisha kuendelea kushika dola.
Alisema Polisi wametanda kila kona kwa sasa hivyo amani itarejea.
Zena alisema homa na
mtikisiko uliopo kwenye wilaya ya Kibiti na Rufiji inaumiza jamii hasa
wanaccm na viongozi wake ambao hawaishi kwa raha saa 12 jioni inabidi
waingie ndani kujifungia.
Aliyekuwa katibu wa CCM
mkoani Pwani anaesubiri makabidhiano, Hassan Mtenga, alitoa pole na
kusema amepokea changamoto hiyo na ataikabidhi kwa katibu aliyeteuliwa
sasa Anastasia Amas.
Ni matukio takriban 11
ya mauaji ya viongozi mbalimbali wa chama, wenyeviti wa vijiji na
vitongoji ambayo yanadaiwa kujitokeza wilayani Rufiji na Kibiti.
Katika matukio hayo ni
pamoja la March 28 ambapo mwenyekiti wa (CCM) tawi la Mparange na
mjumbe wa serikali ya kijiji cha Ikwiriri Kaskazini ,wilayani Rufiji
mkoani Pwani, Michael Lukanda,aliuawa kwa kupigwa risasi ya kichwani na
watu wasiojulikana.
Jingine ni march 12,mwenyekiti wa kitongoji cha Kazamoyo Hemed Njiwa aliuawa kwa kupigwa risasi.
Jan 19,mjumbe wa serikali ya kijiji cha Nyambunda ,Oswald Mrope, aliuawa kwa kupigwa risasi.
March 1,mwenyekiti wa kijiji cha Nyambunda Said Mbwana aliuawa.
Feb 24,watu watatu akiwemo afisa upelelezi wa polisi wilaya ya Kibiti Peter Kubezya aliuawa kwa risasi.
Octoba 24,2016 afisa
mtendaji wa kijiji cha Nyambunda Ally Milandu alipigwa risasi na kufa na
novemba 6,2016 ,mwenyekiti wa kitongoji cha Nyang’unda kijiji cha
Nyambunda Mohammed Thabiti alipigwa risasi akielekea kwake.
Jeshi la polisi Pwani na
serikali mkoani hapa, linaendelea kupambana kufuatia matukio hayo na
kuimarisha ulinzi ikiwemo kusitisha usafiri wa bodaboda ifikapo saa 12
jioni.
No comments :
Post a Comment