Aliyekuwa Mwandishi wa Habari wa Channel Ten mkoa wa Geita,Vallence Robert Amefariki dunia Hii Leo Tarehe 28/03/2017, akiwa nyumbani kwao Muleba Kagera. Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake Ribarikiwe..
Mwenyekiti
wa Klabu ya waandishi wa habari Mkoa wa Geita Daniel Limbe
amethibitisha taarifa za kifo cha mwandishi wa habari Valence Robert.
Limbe ameiambia Maduka online kuwa Valence Robert hivi karibuni aliondoka mkoani Geita akiwa anaumwa.
Hata hivyo inaelezwa kuwa Valence Robert alikuwa anaumwa ugonjwa usiojulikana.
Mazishi yanatarajiwa kufanyika kesho nyumbani kwao Misenyi.
Hivi
karibuni Valence Robert na Joel Maduka walipigwa na askari polisi
wakati wakiwatawanya wananchi kwenye maeneo ya stendi ya zamani Mjini
Geita ambao walikusanyika kusalimiana na Waziri mkuu mstaafu ambaye pia
ni mjumbe wa kamati kuu Taifa ya Chadema Edward Lowassa.
No comments :
Post a Comment