Timu ya Singida
imefanikiwa kuwasajili wachezaji wengine Wazimbabwe Elisha Muroiwa mweye
umri wa miaka 27 na Wisdom Mtasa 22 kwenye kikosi chao kinachojiandaa
na Ligi Kuu Bara.
Katibu Mkuu wa
Singida, Abdulrahman Simba amelithibitisha hilo kwa kuwasajili nyota hao
Muroiwa anayecheza nafasi ya kiungo mkabaji namba 6 ambaye yupo kwenye
kikosi cha timu ya Taifa ya Zimbabwe iliyokuwa inashiriki Afcon, mwaka
huu.
“Ni kweli tumewasajili
kabisa leo Singida tumesajili Wazimbabwe wawili mikataba ya miaka
miwili ambao ni Muroiwa anayecheza namba 6 aliyekuwepo kwenye timu ya
taifa ya Zimbabwe iliyoshiriki Afcon, mwaka huu na Mtasa anayecheza
namba 8 na 10 yeye yupo kikosi cha timu ya taifa cha vijana cha
U23,”alisema Sima.
No comments :
Post a Comment