Mkuu
wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akijitwisha ndoo ya maji baada
ya kuzindua mradi wa maji wa kijiji cha Iguguno wilaya ya Mkalama ikiwa
ni maadhimishi ya kilele cha wiki ya maji yaliyofanyika katika kijiji
hicho cha Iguguno, kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya Mkalama Injinia Jakson
Masaka.
Mkuu
wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akimtwisha ndoo ya maji mkazi wa
kijiji cha Iguguno wilaya ya Mkalama Bi Joyce ikiwa ni sehemu ya
maadhimisho ya kilele cha wiki ya maji.
Mkuu
wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akihutubia baadhi ya wananchi wa
kijiji cha Iguguno Wilaya ya Mkalama kwenye maadhimishio ya kilele cha
wiki ya maji. Pamoja na mambo mengine Dkt. Nchimbi ameagiza askari wa
usalama barabarani kupanda miti ya matunda ili waweze kula matunda
kuboresha afya za macho yao waweze kuona vizuri kipindi wanatekeleza
majukumu yao barabarani.
…………..
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.
Rehema Nchimbi amewaagiza watendaji wa serikali kuanzia ngazi ya
kitongoji hadi Mkoa kusimamia na kuwa walinzi wa kwanza wa miundombinu
ya
miradi yote inayotekelezwa na serikali pamoja na wahisani hasa
miundombinu ya maji ambayo imekosa usimamizi wa kutosha.
Dkt. Nchimbi ametoa agizo hilo
katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya maji mara baada ya kusimamia
makabidhiano ya mradi wa maji ulioibuliwa na halmashauri ya Iramba kabla
ya kuundwa kwa halmashauri ya Mkalama ulipo mradi wa maji wa Iguguno
wenye thamani ya shilingi milioni 847,099,550 na unahudumia watu elfu
kumi.
Amesisitiza kuwa serikali na wadau
mbalimbali wamekuwa wakitumia fedha nyingi kutengeneza miradi ya maji
ili kuwapunguzia wananchi adha ya upatikanaji wa maji safi na salama
ambapo miradi hiyo imekuwa haileti mafanikio yaliyotarajiwa kutokana na
kukoa usimamizi wa kutosha.
“Naelekeza taarifa ya miradi yote
ya maji iletwe ofisini kwangu, nataka nifahamu miradi ambayo imefikia
lengo la kuwapatia wananachi maji na ile ambayo wananchi hawajaanza
kunufaika kwa kupata maji safi na salama lakini fedha za umma
zimetumika”, amesema Dokta Nchimbi.
Aidha, Dkt. Nchimbi amewaaigiza
watendaji wa vijiji na kata kusimamia na kutunza miundo mbinu mbalimbali
ikiwemo ya maji katika maeneo yao huku akielekeza kuwa endapo uharibifu
utatokea mtendaji aliyepo katika eneo husika atawajibishwa kwa uzembe.
Awali Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.
Nchimbi ametembelea chanzo cha maji cha Mwankoko kinachotoa maji katika
halmashauri ya manispaa ya Singida na kisha kupanda miti ili kutunza
mazingira na kuhifadhi chanzo hizo.
Akitoa taarifa ya chanzo hicho,
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (SUWASA)
mjini Singida Hosea Maghimbi amesema zaidi ya shilingi bilioni 1.5 sawa
na asilimia 99.2 kwa kipindi cha mwaka wa fedha wa 2016/17 kwa ajili ya
fidia kwa wakazi walio jirani na chanzo hicho.
Maghimbi amesema SUWASA iko katika
ujenzi wa mradi wa mtandao wa maji na mfumo wa maji safi Singida mjini
pamoja na kuboresha huduma ya maji kwa miji midogo ya Manyoni na
Kiomboi.
Amesema baadhi ya changamoto
zinazokabili SUWASA ni pamoja na wateja kutolipa madeni kwa wakati
hasa taasisi za serikali, wateja wanaokatiwa huduma kwa sababu ya
madeni kutorejeshewa huduma hizo na badala yake kununua maji kwa
majirani, kujifungia maji na kuchepusha dira za maji.
Maghimbi ametoa wito kwa wananchi
kutokata miti, kuchoma moto, kuchungia mifungo na kufanya shughuli
zangine za binadamu kwenye vyanzo vya maji.
“Nitumie nafasi hii kuwaomba
wananchi kufichua watu wanaojiunganishia maji kiholela, wanaojifungia
maji na kuchepusha dira ya maji, kwamba SUWASA inatoa zawadi ya
shillingi 50,000 kwa ye yote atakayetoa taarifa sahihi kuhusiana na watu
hao, ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria”, amesema Maghimbi
No comments :
Post a Comment