Mbunge
wa jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akizungumza na madiwani wa
halmashauri hiyo katika baraza la madiwani. (picha na Mwamvua Mwinyi)
Na Mwamvua Mwinyi, Chalinze
MBUNGE wa jimbo la
Chalinze Ridhiwani Kikwete pamoja na madiwani wa halmashauri ya
Chalinze
,wameujia juu uongozi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira
Chalinze CHALIWASA kwa kushindwa kusambaza maji ili kuondoa kero hiyo .
Amesema mradi huo ulitakiwa kukabidhiwa mwezi huu jimboni hapo lakini unasuasua.
Ridhiwani aliyasema hayo kwenye baraza la Madiwani lililofanyika Lugoba.
Alisema tatizo la ukosefu wa maji, bado ni kubwa hivyo inaonekana uongozi wa Mamlaka hiyo umeshindwa kutatua.
Ridhiwani alifafanua
kwamba hadi sasa hakuna matenki yaliyojengwa na mabomba hayajafukiwa
hivyo ni ndoto za alinacha mradi huo kukamilika mwezi huu.
Kwa mujibu wake, waziri
wa maji anapaswa kulieleza bunge na wananchi wa Chalinze fedha za maji
zilizopelekwa kwa ajili ya mradi huo na mwezi wa kuumaliza .
“Kama mradi huu
utaendelea kusuasua wananchi na wawekezaji wanaokimbilia kuwekeza
Chalinze watashindwa kutimiza malengo yao na kuendelea kuishi kwenye
adha hii inayowapa wakati mgumu “alisema Ridhiwani.
Nao madiwani walisema, kama uongozi wa mamlaka hiyo umeshindwa kazi basi wawapishe .
Diwani wa Lugoba, Rehema Mwene,aliiomba serikali imsimamie mjenzi wa mabomba na matenki amalize kazi hiyo.
Nae Hassan Mwinyikondo,
alieleza hatari kubwa kwa wananchi wa maeneo ya Bwilingu na Chalinze
ambao wanatumia maji yasiyo safi wala salama.
Alisema mradi wa maji wa CHALIWASA hauna faida, kutokana na wananchi kukosa maji kwa kipindi kirefu.
Hussein Hading’oka
aliweka hofu katika kipindi kinachokuja kuwa cha mvua za masika na
kuongeza kwamba mara kadhaa viongozi wa CHALIWASA wamekuwa wakisema
kipindi cha mvua mitambo yao huwa inasumbuliwa na tope.
hivyo kushindwa kufanyakazi za kusukuma maji.
Alimshangaa Meneja wa
Mamlaka hiyo Mhandisi Christer Mchomba kushindwa kuhudhuria kikao hicho
kama alivyotakiwa na Mkurugenzi Edes Lukoa .
Meneja huyo alitakiwa
kwa ajili ya kuwapatia Madiwani hao maelezo ya kina kuhusiana na tatizo
sugu la maji linalowakabili wananchi wa Halmashauri hiyo kwa miaka mingi
sasa.
Mkurugenzi wa
Halmashauri hiyo, Edes Lukoa alisema Halmashauri imetenga bajeti iwa
ajili ya maeneo ambayo hayafikiwi na CHALIWASA hivyo mamlaka hiyo lazima
iwe na mpango wake.
Hivi karibuni Waziri wa
Mazingira Januari Makamba alipofanya ziara ndani ya Halmashauri hiyo
alifika eneo la chanzo cha maji Wami na kutoa maagizo kwa wilaya na
mkoa.
Aliagiza Mkuu wa wilaya
Alhaj Hemed Mwanga kuhakikisha na Mkoa wanakutana na wenzao wa Morogoro
kuzungumzia suala la wafugaji wanaotokea Morogoro kuvamia kando ya mto
WAMI na kuhakikisha wakulima wanaolima kando ya mto wondolewe mara moja.
No comments :
Post a Comment