Saturday, March 25, 2017

BALOZI PHILIP SANKA MARMO AAGWA NA BABA MTAKATIFU PAPA FRANCIS BAADA YA KUMALIZA MUDA WAKE


ARO
Aliyekuwa balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Philip Marmo ameagwa
rasmi jana na viongozi wa Vatican, balozi huyo aliyekuwa na makazi
yake jijini Berlin, alikuwa anahudumu nchi 10 na nafasi yake hivi sasa
itashikiliwa na balozi Abdalah Possi ambaye aliapishwa jana na Rais Dk
John Magufuli.
Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani aliyemaliza muda wake, mheshimiwa
Philip Sanka Marmo ambaye alikuwa anahudumia nchi 10 ikiwemo Vatican,
akiagana na Baba Mtakatifu Papa Francis jana baada ya kustaafu
utumishi wake, (kulia) ni mke wake mama Nuruana Marmo.
ARO 1
Baba Mtakatifu wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis akimpa zawadi
mama Nuruana Marmo, mke wa Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, balozi
Philip Marmo aliyemaliza muda wake ambaye alikuwa anahudumia nchi 10
ikiwemo Vatican, mama Nuruana Marmo, wakati walipofika jana kwa ajili
ya kumuaga Papa.
ARO 3
Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani aliyemaliza muda wake Philip Marmo
akiagana jana na Mkuu wa Utawala, Vatican (Secretary of State),
Mhadhama Kardinali Pietro Parolin, balozi Marmo alikuwa anatumikia
nchi 10 ikiwemo Vatican.
ARO
Balozi Philip Marmo akiagana na Mkuu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano na
Mataifa (Secretary for Foreign Relations with States), Askofu Mkuu
Paul Callagher, alipofika jana kuagana na viongozi wa Vatican, balozi
Marmo ambaye alikuwa na makazi yake jijini Berlin nchini Ujerumani
alikuwa anahudumia nchi 10 ikiwemo Vatican.

No comments :

Post a Comment