Na Greyson Mwase, Dar es Salaam
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Nishati na Madini, Profesa James Mdoe amewataka wananchi kuwa wavumilivu
wakati Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) likifanya jitihada za
kufanya uchunguzi katika mfumo mzima wa Gridi ya Taifa na kurekebisha
hitilafu
iliyopelekea kukosekana kwa umeme katika mikoa yote
iliyounganishwa na Gridi ya Taifa.
Profesa Mdoe aliyazungumza hayo
leo katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam
wakati akielezea tukio la kukatika kwa umeme katika mikoa yote
iliyounganishwa na Gridi ya Taifa asubuhi majira ya saa moja
Alisema mara baada ya wataalam
kutoka Tanesco kugundua hitilafu, wataalam walianza kushughulikia tatizo
hilo na kufanikisha kurejesha umeme katika mikoa ya Iringa ambayo
ilipata umeme saa 1:27, Dar es Salaam saa 1: 43 pamoja na Zanzibar
ambayo ilipata umeme saa 2: 42 na kuongeza kuwa ilipofika saa 2:50 mikoa
yote iliyounganishwa na Gridi ya Taifa ilipata umeme.
Alieleza kuwa uwashaji wa mitambo unaendelea na uchunguzi wa kubaini chanzo cha hitilafu bado unaendelea.
Wakati huo huo Mkurugenzi Msaidizi
katika Masuala ya Usafirishaji Umeme Mhandisi Kahitwa Bishaija alisema
mpaka sasa tatizo limeshadhibitiwa
No comments :
Post a Comment