Katibu wa Bodi ya Wadhamini ya
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji
wa JKCI Prof. Mohamed Janabi akisoma taarifa ya Taasisi katika kikao cha
kwanza cha Bodi hiyo kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kushoto
ni Mwenyekiti wa Bodi ambaye pia ni Daktari Bingwa wa upasuaji wa
Magonjwa ya Moyo na mishipa ya damu Prof. William Mahalu.
Mwenyekiti wa Bodi ya
Wadhamini ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambaye pia ni
Daktari Bingwa wa upasuaji wa Magonjwa ya Moyo na mishipa ya damu Prof.
William Mahalu akiongoza kikao cha kwanza cha bodi hiyo kilichofanyika
leo jijini Dar es Salaam.
Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini
ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakifuatilia taarifa ya
Taasisi hiyo iliyokuwa ikisomwa na Katibu ambaye pia ni Mkurugenzi
Mtendaji wa JKCI Prof. Mohamed Janabi katika kikao cha kwanza cha Bodi
kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Anna Nkinda – JKCI
No comments :
Post a Comment