Waziri wa Afya Mahmoud Thabit
Kombo (kushoto) akiwa na Balozi wa Palestina Nchini Tanzania Hazem
Shabat wakitiliana saini makubaliano ya ushirikiano ambapo Wizara ya
Afya itapatiwa misaada ya kitaaluma kutoka Palestina. Picha na Makame
Mshenga-Maelezo.
…………….
Na Ramadhani Ali/Maelezo Zanzibar
Wizara ya Afya imetiliana saini na
Jamhuri ya watu wa Palestina makubaliano mapya ya mashirikiano ya miaka
mitano ambapo Palestina itaipatia Wizara msaada wa mafunzo kwa
madaktari na wafanyakazi wa kada nyengine.
Waziri wa Afya Mahmoud Thabit
Kombo alitia saini kwa niaba ya Wizara na Palestina iliwakilishwa na
Balozi wa Nchi hiyo Tanzania Hazem Shabat.
Akizungumza katika shehere hiyo
iliyofanyika Wizara ya Afya Mnazimmoja, Waziri wa Afya alisema kupitia
mashirikiano hayo mapya Palestina wameonyesha hamu kubwa ya kusaidia
masuala ya taaluma kwa wafanyakazi wa Wizara hiyo.
Amesema Palestina imekuwa rafiki
mkubwa wa Zanzibar lakini mashirikiano hayo mapya yatapanua wigo mpana
zaidi wa missada yake ambayo itawanufaisha wananchi
Alisema kwa kuanzia madaktari
kutoka Palestina wataweka kambi ya matibabu ya maradhi mbali mbali
Zanzibar kwa kushirikiana na madaktari wazalendo kuanzia mwezi Ogasti
mwaka huu.
Aliongeza kuwa Madaktari wa
Zanzibar watapata fursa ya kwenda Palestina na wao kuja Zanzibar kwa
lengo la kubadilisha uzoefu na kujifunza katika taaluma hiyo.
Naye Blozi wa Palestina nchini
Tanzania Hazem Shabat alisema mashirikiano ya nchi yake na Tanzania
yalianza tokea wakati wa Mwalimu Nyerere ambapo Madaktari bingwa kutoka
Palestina walikuwa wakija kusaidia matibabu.
Alisema makubaliano mapya ya sasa
ni kuzidi kuimarisha mashirikiano hayo na kuahidi kuwa nchi yake
itaongeza ushirikiano katika sekta nyengine zikiwemo
No comments :
Post a Comment