Sunday, March 26, 2017

POLEPOLE AZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI

01
02
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole, akzungumza na Waandshi wa habari katika Ukumbi wa Sekretarieti, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam,leo.
(Picha na Bashir Nkoromo)
 
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole, akzungumza na Waandshi wa habari katika Ukumbi wa Sekretarieti, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam,leo. (Picha na Bashir Nkoromo)
 
Uteuzi wa Makatibu wa CCM Mikoa...

1 Arusha - Elias Mpanda
2 Dar - Saad Kusilawe
3 Dodoma - Jamila Yusuf
4 Geita - Adam Ngalawa
5 Iringa - Christopher Magala
6. Kagera- Rahel Degeleke
7. Katavi- Kajoro Vyahoroka
8. Kigoma- Naomi Kapambala
9. Kilimanjaro- Jonathan Mabihya
10. Lindi-Mwanamasoud Pazi
11. Manyara -Paza Mwamlima
12. Mara -Innocent Nanzabar
13. Mbeya -Wilson Nkhambaku
14. Morogoro- Kulwa Milonge
15. Mtwara -Zacharia Mwansasu
16. Mwanza- Raymond Mwangala
17. Njombe- Hossea Mpagike
18. Pwani- Anastanzia Amasi
19. Rukwa- Loth Ole Nesere
20. Ruvuma- Amina Imbo
21. Shinyanga -Haula Kachambwa
22. Simiyu- Donald Etamya
23. Singida- Jimson Mhagama
24. Tabora- Janeth Kayanda
25. Tanga- Allan Kingazi.

"Makatibu wengi tuliowateua ni wapya, hatuwezi kufanya mageuzi ya kuwa na CCM mpya na upya huo usionekane. Mageuzi ni fikra...

'Kuhusu suala la Mkuu mkoa mkoa wa DSM, kwanza napenda kusema kuwa uhusiano wa CCM na vyombo vya habari ni wa kihistoria'...

CCM inapenda kufuata utaratibu na ndio salama yetu kama yupo kiongozi wa chama amefanya jambo tuna utaratibu mzuri wa kuchunguza'..

'Mkuu wa mkoa ni mteule wa Rais na anapomteua anamteua yeye peke yake na halazimiki kushauriana na mtu'..

"  Humphrey Polepole
Katibu wa CCM itikadi na Uenezi -Taifa
26.3.2016

Profesa Justin Ntalikwa


Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania,  Jenerali Venance Mabeyo akizungumza na wanahabari kuhusu Jeshi hilo kuanza kulipa deni wanalodaiwa na Shirika la Umeme nchini TANESCO kuanzia Machi 28. Mkutano huo umefanyika katika Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi Ngome jijini Dar es Salaam leo Machi 26, 2017.
NA K-VIS BLOG
MKUU wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo, amesema JWT itapunguza deni lake la umeme inalodaiwa na Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), kuanzia Machi 27, 2017.
Akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya JWTZ, Ngome Upanga jijini Dar es Salaam, leo Machi 26, 2017, Mkuu huyo wa Majesho alisema, “tayari nimeshaagiza idara husika kuandika hundi na kuiepeleka TANESCO Machi 27, 2017 ili kupunguza deni tunalodaiwa na Shirika letu la umeme linalozidi kidogo Shilingi Bilioni 3.” Alisema Jenerali Mabeyo.
Mkuu huyo wa Majeshi alisema, “Natoa wito kwa taasisi nyingine kulipa madeni ya TANESCO ili tuliwezeshe shirika letu liwe na uwezo wa kutoa huduma kwa uhakika na hivyo kuwawezesha wananchi kuwa na uhakika wa kupata umeme.” Alisema Jenerali Mabeyo.
Rais John Pombe Magufuli, akizindua ujenzi wa kituo cha kupoza na kusambaza umeme huko Mtwara cha umeme wa 133Kv, aliagiza Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO) kukata umeme kwa wadaiwa sugu. “Hata kama Ikulu wanadaiwa umeme, kata, hata Jeshi, polisi na kwingineko, wewe kata.” Alisagiza Rais Magufuli.
Baada ya agizo hilo la Rais, uongozi wa Shirika hilo uliitisha waandishi wanhabari na kutoa siku 14 kwa wadaiwa wote kulipa madeni yao  vinginevyo huduma ya umeme ingesitishwa baada ya muda huo.
JWTZ, inakuwa taasisi ya kwanza nyeti kutoka hadharani na kuahidi kupunguza deni hilo la umeme, tayari Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO), nalo limeahidi kupunguza deni la umeme.

No comments :

Post a Comment