Chama cha watu wenye ualbino nchini
(Tanzania Albinism Society-TAS) kimeanza kampeni ya kutoa elimu kuhusu
masuala ya ualbino katika nyumba za ibada ambapo leo viongozi wa chama
hicho taifa wametoa elimu katika kanisa la KKKT Usharika wa Ebenezer
Kanisa Kuu Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria lililopo mjini
Shinyanga.
Viongozi hao wakiongozwa na Afisa
Mahusiano na Habari kutoka TAS ,Josephat Torner wametoa elimu kuhusu
mambo ya ualbino kanisani hapo wakati wa ibada ya Jumapili leo Machi
26,2017.
Akizungumza kanisani hapo Torner alisema
kampeni hiyo inalenga kutoa elimu kwa jamii kuhusu masuala ya ualbino
kwa viongozi wa dini na waumini wao na wanaendelea pia kutoa elimu hiyo
kwa makundi mengine ya watu katika jamii wakiwemo waganga wa kienyeji.
“Tumeona vita hii tunayopambana nayo
bila kumjua hasa adui ni nani,ni vyema elimu iwafikie watu wengi zaidi
na tunaamini kupitia nyumba za ibada jamii itakuwa na uelewa wa kutosha
juu ya masuala ya ualbino ili kukabiliana na tatizo la mauaji ya watu
wenye ualbino na hata vitendo vya kufukua makaburi ya watu wenye ualbino
vinavyoendelea kujitokeza nchini”,alieleza Torner.
Alisema bado watu wengi hawana elimu ya
kutosha kuhusu masuala ya ualbino hali inayosababisha kuongezeka kwa
unyanyapaa ambapo sasa hata wamiliki wa nyumba za kupanga wanawanyima
vyumba watu wenye ualbino wakihofia kupata matatizo.
“Nyumba za ibada zina watu
wengi,tutapita kwenye makanisa na misikiti kutoa elimu hii ili viongozi
na waumini waelewe hasa maana ya ualbino ili tuungane pamoja kutokomeza
vitendo vya kikatili dhidi ya watu wenye ualbino”,aliongeza Torner.
“Kutokana na imani potofu katika
jamii watu wenye ualbino wanaishi kwenye vituo maalum,wanaishi kwa hofu
kubwa ya kuuawa na sasa kuna baadhi ya watu wameanza kufukua makaburi ya
watu wenye ualbino hivyo kunahitajika jitihada zaidi katika kupambana
na ukatili huu”,alisema Torner.
Alisema mbali na jitihada zinazofanywa
na serikali katika mapambano dhidi ya ukatili huo ni vyema jamii ikatoa
ushirikiano katika kupiga vita vitendo hivyo vya kikatili.
Akizungumza kwa niaba ya uongozi wa
kanisa hilo,Mchungaji Jackson Maganga alisema kanisa hilo lina programu
nyingi za kutoa elimu kwa waumini wake juu ya vitendo vya ukatili kwa
watu wenye ualbino na kwamba kanisa hilo liko tayari kushirikiana na
chama hicho katika mapambano dhidi ya ukatili kwa watu wenye ualbino.
Mwandishi mkuu
wa Malunde1 blog,Kadama Malunde alikuwepo wakati wa ibada ya Jumapili
katika kanisa hilo,ametusogezea picha 23 za matukio yaliyojiri..Tazama
hapa chini
Mchungaji Geofrey Kaijunga akitoa
mahubiri katika ibada ya Jumapili katika kanisa la KKKT Usharika wa
Ebenezer Kanisa Kuu Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria
lililopo mjini Shinyanga.
Mchungaji Geofrey Kaijunga aliwataka
waumini wa kanisa hilo kumtegemea mungu kwa kila jambo huku akisisitiza
kuwa thamani ya mtu hupanda pale anapookoka
Ibada ya Jumapili katika kanisa la KKKT Usharika wa Ebenezer Kanisa Kuu Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria ikiendelea
Mchungaji Jackson Maganga wa kanisa la
KKKT Usharika wa Ebenezer Kanisa Kuu Dayosisi ya Kusini Mashariki ya
Ziwa Victoria, akiwakaribisha kanisani viongozi wa chama cha watu wenye
ualbino nchini Tanzania
Afisa Programu kutoka chama cha watu
wenye ualbino Tanzania Severin Edward akiteta jambo na Afisa Mahusiano
na habari kutoka chama cha watu wenye ualbino Tanzania (TAS)Josephat
Torner
Kushoto ni Mkurugenzi wa wanawake,Watoto
na Diakonia katika kanisa la KKKT Usharika wa Ebenezer Kanisa Kuu
Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria,Martha Ernest Ambarang’u
akiwatambulisha viongozi kutoka TAS.Wa pili kutoka kushoto ni Afisa
Programu kutoka TAS Severin Edward ,akifuatiwa Happiness Ngaweje na
afisa mahusiano na habari (TAS)Josephat Torner
Afisa Mahusiano na habari kutoka chama
cha watu wenye ualbino Tanzania (TAS) Josephat Torner akitoa elimu
kuhusu masuala ya ualbino katika kanisa la KKKT Usharika wa Ebenezer
Kanisa Kuu Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria
Afisa Mahusiano na Habari kutoka TAS,Josephat Torner akizungumza kanisani
Waumini wakimsikiliza Afisa Mahusiano na habari kutoka chama cha watu wenye ualbino Tanzania (TAS) Josephat Torner
Afisa Mahusiano na habari kutoka chama
cha watu wenye ualbino Tanzania (TAS) Josephat Torner akiendelea kutoa
elimu kuhusu masuala ya ualbino huku akiitaka jamii kutoa ushirikiano wa
dhati katika mapambano dhidi ya ukatili kwa watu wenye ualbino
Afisa Mahusiano na habari kutoka chama cha watu wenye ualbino Tanzania (TAS) Josephat Torner akizungumza kanisani
Waumini wakipa somo kuhusu masuala ya ualbino
Mchungaji Jackson Maganga wa kanisa la
KKKT Usharika wa Ebenezer Kanisa Kuu Dayosisi ya Kusini Mashariki ya
Ziwa Victoria akieleza namna kanisa hilo linashiriki katika mapambano
dhidi ya ukatili kwa watu wenye ualbino
Mchungaji Jackson Maganga akizungumza kanisani
Waumini wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea kanisani
Mchungaji Goodluck Mosha akizungumza jambo kanisani
Wachungaji wa kanisa la KKKT Usharika wa Ebenezer Kanisa Kuu Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria
Viongozi wa TAS wakiwa kanisani
Waumini wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea kanisani
Waumini wa kanisa la KKKT Usharika wa
Ebenezer Kanisa Kuu Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria wakiwa
nje ya kanisa baada ya ibada kumalizika
Viongozi wa TAS wakiondoka katika kanisa la KKKT Usharika wa Ebenezer Kanisa Kuu Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria
Kanisa la KKKT Usharika wa Ebenezer Kanisa Kuu Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
No comments :
Post a Comment