Wizara ya Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi kwa kushirikiana na Kampuni ya udalali ya Msolopa
inatoa taarifu kwa wananchi wote kuwa zoezi la mnada lililotarajiwa
kufanyika Jumapili – tarehe 26/03/2017 halitafanyika tena kwa sababu
wadaiwa wote wa viwanja vilivyokuwa vinadiwe kutokana na kuwa na madeni
sugu ya kodi ya pango la ardhi, wametimiza masharti ya malipo kabla ya
siku ya mnada kufanyika.
Aidha, orodha ya viwanja vingine
vya maeneo ya Kinondoni, Temeke na Ilala vyenye madeni sugu ya Kodi ya
pango la ardhi itatolewa kuanzia wiki ijayo.
LIPA KODI YA PANGO LA ARDHI KWA WAKATI
Usipolipa Kodi ya Pango la Ardhi,
utanyang’anywa umiliki wa Ardhi yako, kutokana na sheria ya Ardhi, Na. 4
ya mwaka 1999, katika kifungu cha 49 na 51.
Kodi ya ardhi hulipwa kila
ifikapo Julai Mosi ya kila Mwaka katika Manispaa au Halmashauri husika
na katika Ofisi za Malipo ya Kodi – Dar es Salaam
Imetolewa na:
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
No comments :
Post a Comment