Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afaya
Zanzibar Dkt. Fadhil Mohammed Abdalla akieleza mipango iliyoandaliwa
ya kukabiliana na maradhi ya kipindupindu iwapo yatatokezea katika
kikao kilichofanyika Hospitali ya wagonjwa wa akili Kidongo chekundu
Mjini Zanzibar.
Mkuu wa Kitengo cha Afya ya
Mazingira Rukaiya Mohamed Said akiwasilisha taarifa ya kikao kilichopita
cha Kamati hiyo kilichofanyika mwezi uliopita.
Afisa kutoka Jumuia ya watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi Zanzibar Jokha Masoud Salim akitoa mchango wakati wa kikao hicho.
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa
Kamati ya kukabiliana na kipindupindu wakifuatilia kikao hicho
kilichofanyika Hospitali ya wagonjwa wa akili Kidongochekundu.
Afisa uperesheni na huduma za
kibinadamu, Kamisheni ya kukabiliana na maafa Makame Khatibu Makame
akitoa mada juu ya mpango wa kukabiliana na maafa Zanzibar katika cha
Kamati hiyo kilichofanyika Hospitali ya wagonjwa wa akili
Kidongochekundu.
Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
………………
Na Khadija Khamis –Maelezo
Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya
Dkt Fadhil Moh’d Abdalla ameitaka jamii kubadili tabia
kwa kuweka
mazingira yaliyowazunguka safi na kuhakikisha wanatumia maji safi na
salama ili kujiepusha na maradhi ya mribuko .
hayo ameyasema wakati wa kikao
cha kamati ya kitaifa ya kuandaa mpango mkakati wa kudhibiti maradhi ya
kipindupindu hasa kipindi hichi ambacho mvua za masika zimeanza
kunyesha.
Alisema lengo kuu la kamati hiyo
ni kufanya tadhmini ya muendelezo wa mpango kazi wa kudhibiti maambukizi
ikiwemo kutoa elimu ya usafi wa mazingira kwa jamii na kupambana na
mazingira hatarishi katika maeneo mbali mbali ya Manispaa ya Zanzibar.
Ameishauri Mamlaka ya Maji
Zanzibar (ZAWA) kuhakikisha maji yanayotumiwa na wananchi yapo katika
hali ya safi na salama kwa kutia dawa vianzio vyote vya maji na
kuwataka wananchi kuacha tabia ya kufanya uharibifu kwenye njia za maji
kwa kutoboa mabomba yanayosamba maji .
Alieleza changamoto zinazowakabili
kwa sasa ni kuwepo kwa wafanyabiashara wasiofuata taratibu za usafi wa
chakula na mazingira katika utendaji mzima wa biashara zao.
Alisema uzoefu unaonyesha maradhi
ya kipindupindu mara nyingi hutokea wakati wa kipindi cha mvua hivyo
tahadhari zinahitajika katika kuweka mazingira katika hali ya usafi
“Wananchi wahakikishe wanakunywa
maji ya kuchemsha au kuyatia watergard ili kuweka tahadhari wakati huu
wa kipindi cha mvua za masika kwani kunauwezekano mkubwa wa kuchafuka
vyanzio vya maji kwa kuingia maji machafu,” Alisema Mkurugenzi kinga .
Aliwashauri wananchi wanaoishi
sehemu za mabondeni kuchukue juhudi za makusudi kuhama katika maeneo
hayo ili kuepuka majanga katika kipindi hichi cha mvua za masika
No comments :
Post a Comment