Tuesday, March 28, 2017

HALMASHAURI YA MJI YAKABIDHI VYOO VYA KISASA KWENYE SHULE ZA MSINGI .


KISA
Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Geita,Mhandisi Modest Aporinali akizindua vyoo vya kisasa vya wanafunzi wa shule ya Msingi Mbugani.

Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Geita,Mhandisi Modest Aporinali  akiongozana na mwenyekiti wa kamati ya shule ya msingi Mbugani kwenda kukagua vyoo hivyo.

Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Geita,Mhandisi Modest Aporinali ,akikagua vyoo vya shule ya msingi Mbugani.


Sehemu ya kunawa mikono pindi wanafunzi wanapotoka msalani.

Muonekano wa choo cha kisasa cha kufrashi.

Choo cha watu wenye ulemavu.

Walimu pamoja na wanafunzi wakifatilia kwa makini maelekezo ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji.

Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Geita,Mhandisi Modest Aporinali  akisisitiza jambo kwa walimu na wanafunzi kuvitunza vyoo hivyo.


Halmashauri
ya Mji wa Geita,imekabidhi vyoo vya kisasa kwa shule za msingi za
Nyankumbu,Kivukoni pamoja na Mbugani ambao umegharimu kiasi cha sh,million mia
moja na ishirini.
 
Akielezea
namna ya mradi huo ulivyoanza na kumalizika Mhandisi wa shirika lililokuwa
likisimamia Mradi huo la Acoil Godfey Wandi amesema kuwa mradi huo umefadhiliwa
na Benki ya maendeleo ya Afrika na ujenzi ulianza mwaka 2015 na 2016
ulikamilika na kwamba ni vyoo vya kisasa kwani kuna sehemu za watu wenye
ulemavu.
 
“Kwa sasa
hivi mradi umekamilika na upo tayari kwa ajili ya matumizi kuna majengo mawili
jengo la wasichana na jengo la wavulana na bila shaka leo wanafunzi wanaweza
kuanza kutumia vyoo hivi”Alisema Wandi.
 
Kwa upande
wake Kaimu afisa elimu halmashauri ya Mji wa Geita,Mwl Salome Cherehani  ameishukuru Benki ya maendeleo ya afrika na
kwamba wanaamini kukamilika kwa ujenzi huo utapunguza kero na  adha ambazo zimekuwa zikijitokeza kutokana na
upungufu wa vyoo.

Mkuu wa
shule ya msingi Mbugani Forenci Lernad ,amemweleza mkurugenzi wa halmashauri
hiyo kuwa kutokana na hali ilivyokuwa choo cha shule kilititia na kusababisha
idadi ya matundu ya choo kupungua shuleni hapo.

Hata hivyo
kwa upande wake Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji Mhandisi Modest Aporinali
amewataka walimu pamoja na wanafunzi kuhakikisha wanavitunza vyoo hivyo ili
viweze kudumu.



IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE .

No comments :

Post a Comment