Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijabe (Mb), akizungunza wakati wa Semina iliyoandaliwa
na Taasisi ya Sekta Binafsi hapa nchini-TPSF iliyohusu ugharimiaji
mkubwa wa miradi ya ubia kati ya sekta ya Umma na Sekta Binafsi kupitia
mradi wa TVC (Tanzania Venture Capital and Private Equity Project),
mjini Dodoma
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), (wa pili
kulia) akiandika mambo mawili matatu yaliyojiri wakati wa semina
iliyoandaliwa na Taasisi ya Sekta Binafsi hapa nchini-TPSF iliyohusu
zitaugharimiaji mkubwa wa miradi ya ubia kati ya sekta ya Umma na Sekta
Binafsi kupitia mradi wa TVC (Tanzania Venture Capital and Private
Equity Project), mjini Dodoma
Waziri wa Fedha na Mipango,
Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akihutubia washiriki wa semina
iliyoandaliwa na Taasisi ya Sekta Binafsi hapa nchini-TPSF iliyohusu
zitaugharimiaji mkubwa wa miradi ya ubia kati ya sekta ya Umma na Sekta
Binafsi kupitia mradi wa TVC (Tanzania Venture Capital and Private
Equity Project), mjini Dodoma, ambapo waziri huyo ameitaka sekta binafsi
kuwezesha upatikanaji wa Zaidi ya shilingi Trilioni 48 ili kusaidia
ujenzi wa Miradi Mikubwa ya Maendeleo.
Benny Mwaipaja-WFM, Dodoma
KIASI
cha Shlilingi Trilioni 48 kinahitajika kutoka Sekta Binafsi ili
kufanikisha ujenzi wa miradi mikubwa ya maendeleo kupitia Mpango wa Pili
wa Maendeleo wa Taifa unaotekelezwa kuanzia mwaka wa fedha wa 2016/2017
hadi mwaka 2020/2021
Waziri
wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, amesema hayo mjini Dodoma
wakati akifunga semina ya siku moja iliyoandaliwa na Taasisi ya Sekta
Binafsi hapa nchini-TPS iliyohusu zitaugharimiaji mkubwa wa miradi ya
ubia kati ya sekta ya Umma na Sekta Binafsi kupitia mradi wa TVC
(Tanzania Venture Capital and Private Equity Project)
“Imekadiriwa
kuwa mahitaji ya fedha ya mpango huo ni takriban shilingi Trilioni 107,
kati ya hizo shilingi Trilioni 59, sawa na asilimia 55, zitatokana na
mapato ya Serikali na shiilingi Trilioni 48, sawa na asilimia 45
zitatokana na vyanzo vya Sekta Binafsi.
Amesisitiza
umuhimu wa Sekta Binafsi kuwekeza zaidi kwenye kilimo na viwanda
vitakavyosaidia kuongeza thamani ya mazao ya wakulima ili waweze
kunufaika kiuchumi na kuendeleza nchi kwa ujumla
Dkt.
Mpango, ameahidi kuwa Serikali iko tayari kuhakikisha kuwa vitendea
kazi muhimu vya utekelezaji wa mradi huo vinapatikana ili kuwezesha
utekelezaji wa miradi hiyo ya ubia ukiwemo mradi wa ujenzi wa barabara
ya njia sita kutoka Dar es salaam kwenda Chalinze.
No comments :
Post a Comment