Sunday, February 5, 2017

WAZAZI WATAKIWA KUWAPELEKA WATOTO HOSPITALINI MAPEMA


TUO
Mmoja wa wake wa viongozi, Germina Lukuvi akitoa zawadi kwa watoto wenye saratani katika maadhimisho ya Siku ya Saratani Duniani ambayo yamefanyika Viwanja vya Jakaya Kikwete jijini Dar es Salaam Leo. Kushoto ni  Dk Lodovick ambaye amemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Sofia Mjema.
TUO 1
Watoto wenye saratani hawakuwa nyuma katika maadhimisho hayo kwani wameshiriki na kucheza michezo mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku hii muhimu.
TUO 2
Wazazi wa watoto wenye saratani wakifuatilia michezo mbalimbali iliyokuwa ikichezwa na watoto hao.
TUO 3
Watoto hao wakicheza mchezo wa kuzunguka viti kwenye maadhimisho hayo leo.
TUO 4
Wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili na Chuo Kikuu cha Kairuki wakifuatilia watoto hao wakati wakicheza.
TUO 5
Wanafunzi wakiwa na watoto ha oleo kwenye viwanja vya Jakaya Kikwete jijini Dar es Salaam.
Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)
……………..
 
Dar es Salaam, Tanzania.  Mganga Mkuu Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam, Dk. Victorina Ludovick amewataka wazazi kuwapeleka watoto wao hospitali mapema kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa afya zao.
Kauli hiyo imetolewa leo na Dk Ludovick kwenye maadhimisho ya Siku ya Kansa Duniani ambayo huadhimishwa Februari 04, kila mwaka. Dk Ludovick amemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sofia Mjema katika maadhimisho hayo.
Dk Ludovick amesema kwamba wazazi wanatakiwa kuwapeleka mapema hospitali ili mtoto atakayebainika ni mgonjwa aweze kupatiwa tiba mapema kabla tatizo halijakuwa kubwa.
Pi, Dk Ludovick ameipongeza Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa kuwahudumia watoto wenye saratani bure kwa asilimia 70 wakati asilimia 30 ya gharama za matibabu zinachangiwa na Taasisi ya Tumaini Letu.

No comments :

Post a Comment